Valencia na Tottenham Hotspur wamekubaliana mshambuliaji Roberto Soldado kutua Spurs na wamekamilisha mpango wa uhamisho jana Jumatano.
Mshambuliaji huyo raia wa Hispania mwenye miaka 28 hataruhusiwa kujiunga na Spurs mpaka atakapotatua matatizo na wakala wake.
Rais wa Valencia Amadeo Salvo amesema wamemalizana na Spurs na kinachofuata ni kumaliza matatizo ya Soldado na wakala wake.
Inaelezwa kuwa Spurs wametoa dau la paundi milioni 39.84 kwa Soldado ambaye amezifumania nyavu mara 30 kwenye mechi 46 alizoichezea Valencia msimu uliopita.
Spurs wametumia paundi milioni 25 kumnasa pia kiungo wa Brazil Paulinho kutokea Corinthians mapema mwezi huu.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.