Friday, August 9, 2013
KING'ANG'ANIZI : Mourinho asema mpaka kieleweke kwa Rooney
Boss wa Chelsea Jose Mourinho amesema atapigana mpaka siku ya mwisho kumnasa mshambuliaji wa Manchester United 27,Wayne Rooney.
Mourinho amesema Chelsea haijanyoosha mikono na wala haijakata tama ya kumnasa mshambuliaji huyo na wako tayari kuendelea kumpigaania mpaka wajue mwisho wake.
Tayari Manchester United wamekataa ofa mbili za Chelsea kumtaka Rooney wakiendelea kushikilia msimamo wa kwamba hauzwi.
Mourinho anasema wanafanya mambo kwa kufuata utaratibu na hata ofa wanazotoa wanapeleka moja kwa moja kwa klabu hiyo na hawazungumzi na mchezaji wala hawana mahusiano ya moja kwa moja na mshambuliaji huyo.
Kocha huyo mwenye maneno mengi pia akasema kwamba hawana mpango wowote wa kumuuza beki wao raia wa Brazil David Luiz anayetakiwa na Barcelona.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.