Bingwa wa Wimbledon Marion Bartoli amestaafu kucheza tennis ikiwa ni siku 40 baada ya kushinda taji lake la pekee la Grand Slam.
Bartoli mwenye miaka 28 raia wa Ufaransa anayeshikilia nafasi ya 7 kwenye ubora wa viwango vya dunia kwa wanawake amesema amechukua maamuzi hayo kwasababu ya maumivu aliyonayo na sasa ni wakati wake wa kujiweka pembeni.
Aliangusha machozi wakati akitangaza uamuzi wake mbele ya waandishi wa habari ikiwa ni baada ya kushindwa na Simona Halep kwenye Western and Southern Open huko Cincinnati.
Bartoli,ambaye alimshinda MJerumani Sabine Lisicki kwenye fainali ya Wimbledon mwezi July amesema maumivu mbalimbali yanayomkabili ya,mguu,hips,bega na mamumivu ya mgongo yanayoendelea kila anapocheza ndio yamemuweka pembeni na kuchukua uamuzi huo mgumu.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.