Wednesday, August 21, 2013

Tanzania yashinda medali ya dhahabu

Na Frank Geofray-Jeshi la Polisi,Windhoek Namibia.
Wanariadha wanaowakilisha Jeshi la Polisi Tanzania katika michezo ya Umoja wa wakuu wa Polisi kusini mwa Afrika SARPCCO nchini Namibia wameanza vyema mbio hizo baada ya kufanikiwa kunyakua medali za Dhahabu na fedha katika mbio za mita elfu 10000 wanaume.


Aliyenyakua medali ya dhahabu ni Mwanariadha Fabian Nelson ambaye alitumia dakika 30 na sekunde 42 huku akifuatiwa na Wilbrado Peter (Tanzania) ambaye alitumia dakika 30 na sekunde 45 na kuwaacha wanariadha wengine nyuma kutoka mataifa ya Zimbabwe,Namibia,Botwasana na Angola.

Wengine walioipatia Tanzania Medali ni pamoja na Basili John mita 800 (Shaba ) na Mohamed Ibrahim mchezo wa kurusha kisahani (shaba).

Katika mpira wa miguu mechi ya ufunguzi ilizikutanisha wenyeji Namibia na Msumbiji ambapo Namibia iliichapa Msumbiji mabao 2 kwa 0 huku kwenye mpira wa miguu wanawake Namibia na Angola zilitoka suluhu ya bila kufungana.

Tanzania itaanza kutupa karata yake katika mpira wa miguu dhidi ya Zambia ambapo Tanzania imepangwa kundi B ikiwa na timu za Zambia, Angola ,DRC na Lesotho huku Kundi B lina timu za Namibia, Msumbiji, Botswana na Zimbabwe.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.