Tuesday, August 13, 2013

Etoó aitamani Chelsea,adai Mourinho ni zaidi ya kocha

 
Mshambuliaji Samuel Eto'o ameweka bayana kiu yake ya kutaka kutua Chelsea na kuungana na kocha Jose Mourinho.

Mourinho ameripotiwa kuhitaji huduma ya Eto'o akitaka kunoa makali ya safu yake ya ushambuliaji na mshambuliaji huyo wa Anzhi Makhachkala yuko huru kutimkia kwenye timu hiyo.

Anzhi wameyumba kiuchumi na sasa wameamua kuuza wachezaji wake akiwemo Eto'o anayelipwa dau kubwa.

Eto'o,alikuwa chini ya Mourinho kwenye timu ya Inter Milan,na inaelezwa kuwa Mreno huyo ni shabiki mkubwa wa Etoó na angependa kufanya naye kazi kwa mara nyingine.
Mshambuliaji huyo anasema kuna Mourinho mmoja tu na anasema amecheza chini ya makocha wengi lakini hawana baadhi ya vitu alivyo navyo kocha huyo mchezoni na akimtaja kama mmoja wa makocha bora duniani huku akimwagia sifa Chelsea akisema ni timu kubwa na kama itatua ofa atajadiliana na wakala wake na kuona kinachofuata.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.