Mchezo wa ligi kuu soka Tanzania bara kati ya Yanga na Coastal Union ya Tanga utakaopigwa kwenye uwanja wa Taifa Dar Es Salaam utatangazwa moja kwa moja na kituo cha Radio cha Times fm 100.5 kuanzia saa 10.30 jioni
Kiingilio kwenye mchezo huo itakuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000.
Mwamuzi Martin Saanya wa Morogoro ndiye atakayepuliza filimbi wakati
Kamishna atakuwa Omari Walii kutoka Arusha.
Mechi nyingine za leo Mtibwa Sugar
itaikaribisha Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Manungu ulioko Turiani
mkoani Morogoro wakati Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora utakuwa
mwenyeji wa pambano kati ya wenyeji Rhino Rangers na Azam.
Vumbi lingine litatimka kwenye Uwanja wa Mabatini ulioko Mlandizi mkoani
Pwani wakati maafande wa JKT Ruvu watakapokwaruzana na wenzao wa
Tanzania Prisons kutoka Mbeya. Mbeya City na Ruvu Shooting zitacheza
kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.
Jiji la Tanga litakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Mgambo Shooting na
Ashanti United itakayochezwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani. Oljoro JKT
itakuwa mwenyeji wa Simba kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Kaluta
Amri Abeid jijini Arusha.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.