Friday, August 2, 2013

Chelsea,Real Madrid waendeleza dozi Marekani

Mabao yaliyotumbukizwa wavuni na Oscar Emboaboa na Eden Hazard yamewapa ushindi wa mabao 2-0 Watoto wa darajani Chelsea mbele ya Inter Milan Usiku wa kuamkia leo.

Ushindi huo umeivusha Chelsea mpaka kwenye nusu fainali ambako watakutana na AC Milan Jumapili kwenye dimba la Met Life huko East Rutherford, N.J,wakati Inter watacheza dhidi ya Valencia iliyokula kibano cha mabao 2-1 kutoka kwa AC Milan.
Kocha wa Chelsea Jose Mourinho amekimwagia sifa kikosi chake akisema kimecheza vizuri japo angependa zaidi timu yake ya zamani ya Inter Milan wangekuwa wametimia wote 11.

Anasema kama sheria ingeruhusu Inter kuongeza mchezaji mwingine kutoka nje baada ya mwamuzi kumtoa mchezaji mmoja kwa kadi nyekundu ingekuwa safi zaidi japo akisema sheria za mpira haziruhusu hilo na lazima ziheshimiwe.


Huko GLENDALE, Ariz,
Karim Benzema aliibeba Real Madrid na kuisaidia kupata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Los Angeles Galaxy inayocheza Major League Soccer huko Marekani.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.