Chelsea walitupia mabao yao kupitia kwa kipa wa beki wa Aston Villa aliyejifunga na bao la pili likitupiwa wavuni na Ivanovic huku lile la Aston Villa likifungwa na Benteke.
Kocha wa Chelsea Jose Mourinho na yule wa Aston Villa Paul Lambert walitupiana vijembe baadaye huku Mourinho akimtaka Lambert kuonesha kuwa amekuwa wakati alipokuwa akijaribu kupinga kila maamuzi ya mwamuzi.
Ivanoviv na Benteke walisalimika kutolewa nje kwa kadi nyekundu wakati Ivanovic alipompiga kiwiko Benteke ambaye naye baadaye alirudisha kupiga kiwiko na mwamuzi akamuonya.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.