Friday, August 30, 2013

Azam Tv yaanguka rasmi mkataba wa miaka mitatu na TFF

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na kampuni ya Azam Media leo (Agosti 30 mwaka huu) wamesaini mkataba wa haki za kipekee za televisheni (exclusive rights) utakaoiwezesha Azam TV kuonesha mechi za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL).

Mkataba huo wa miaka mitatu wenye thamani y ash. 5,560,800,000 umesainiwa kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Makamu wa Rais, Athuman Nyamlani amesaini kwa niaba ya TFF wakati aliyesaini kwa upande wa Azam Media ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo Thys Torrington.
Ligi Kuu ya Tanzania sasa itakuwa ikipatikana kupitia kisimbuzi (decorder) cha Azam TV kitakachokuwa na chaneli zaidi ya 50. Mechi hizo zinatarajiwa kuoneshwa moja kwa moja wakati wowote kuanzia mwezi ujao.

Makamu wa Rais wa TFF, Nyamlani amesema udhamini huo wa televisheni ni fursa pana kwa klabu kwani zitaweza kujitangaza zaidi huku wachezaji nao wakipata soko zaidi za mpira wa miguu.

Etoó ndani ya Chelsea,Mourinho meno yote nje,Torres awekwa sokoni

Kutua kwa mshambuliaji Samuel Etoó Fils kutakuwa kumeshusha presha ya kocha wa Chelsea Jose Mourinho The Happy One.

Mourinho alikuwa anasaka mshambuliaji baada ya kutofurahia kazi ya upachikaji mabao inayofanywa na Fernando Torres,Demba Ba na Romelu Lukaku ambao sasa inabidi wakaze mkwiji kama wanataka kuendelea kungára kwenye timu hiyo.
Baada ya kutua kwa mshambuliaji huyo raia wa Cameroon sasa Fernando Torres amewekwa sokoni na Chelsea wako tayari kusikiliza ofa.

Torres amekuwa hana uhakika wa namba tokea alipotua kwenye klabu hiyo kwa dau la paundi milioni 50 lililoweka rekodi ya uhamisho England akitokea Liverpool.
 Licha ya Demba Ba kutakiwa na Newcastle United Mourinho hana uwoga wa kumuuza Torres kwakuwa anaamini Lukaku atakuwa msaada mkubwa kwa timu hiyo na yumo kwenye mipango yake.


Thursday, August 29, 2013

Makundi ya Uefa Champions League Barcelona kundi la kifo

Group A: Manchester United, Shakhtar Donetsk, Bayer Leverkusen, Real Sociedad
Group B: Real Madrid, Juventus, Galatasaray, Copenhagen
Group C: Benfica, Paris St-Germain, Olympiakos, Anderlecht
Group D: Bayern Munich, CSKA Moscow, Manchester City, Viktoria Plzen
Group E: Chelsea, Schalke, Basel, Steaua Bucharest
Group F: Arsenal, Marseille, Borussia Dortmund, Napoli
Group G: Porto, Atletico Madrid, Zenit St Petersburg, Austria Vienna
Group H: Barcelona, AC Milan, Ajax, Celtic

Uefa Champions league ratiba live

Group A: Manchester United, Shakhtar Donetsk, Bayer Leverkusen
Group B: Real Madrid, Juventus, Galatasaray
Group C: Benfica, Paris St-Germain, Olympiakos
Group D: Bayern Munich, CSKA Moscow, Manchester City
Group E: Chelsea, Schalke, Basel
Group F: Arsenal, Marseille, Borussia Dortmund
Group G: Porto, Atletico Madrid, Zenit St Petersburg
Group H: Barcelona, AC Milan, Ajax

Etoó rasmi wa Chelsea


Chelsea wamemalizana na mshambualiji raia wa Cameroon Samuel Eto'o kwa uhamisho wa bure akitokea Anzhi Makhachkala ya Russia.

Etoo aliyesaini mkataba wa mwaka mmoja anasema hayakuwa maamuzi magumu kwake,anaujua ubora wa Chelsea na amekuwa na furaha na kocha wa timu hiyo Jose Mourinho kabla ya kujiungaa na timu hiyo,kwahiyo nafasi inapokuja hawezi kuiacha.

Mourinho amemchukua Eto'o baada ya ofa mbili za Chelsea kuchomolewa na Manchester United ili kumnasa mshambuliaji Wayne Rooney.

Eto'o's club honours

Real Mallorca (1999-2004): Copa del Rey (2003). Scored 69 goals in 165 appearances.

Barcelona (2004-2009): Champions League (2006, 2009); La Liga (2005, 2006, 2009); Copa del Rey (2009); Spanish Super Cup (2006, 2007). Scored 129 goals in 201 appearances.

Inter Milan (2009-2011): Champions League (2010); Serie A (2009); Coppa Italia (2010, 2011), Italian Super Cup (2010); Fifa World Club Cup (2010). Scored 53 goals in 101 appearances.

Anzhi Makhachkala (2011-2013): Scored 36 goals in 71 appearances.

Kundi la kifo Uefa Champions League


Upangaji wa makundi ya michuano ya Uefa Champions league unafanyika baadaye leo huku tayari timu zikiwa zimewekwa kwenye makundi manne yanayoweza kutoa sura ya timu gani inaweza kupangwa na timu gani kwenye hatua ya makundi lakini wengi wakijiuliza nani ataangukia kundi la kifo.

Manchester City inaweza kuangukia kundi moja na Bayern Munich, Atletico Madrid au Paris Saint-Germain, na Napoli.

Lakini Chelsea, Manchester United na Arsenal wako katika hatari ya kuangukia kwenye kundi la kifo na wanaweza kujikuta wapo kundi moja na Atletico au PSG, Borussia Dortmund na Napoli.

Kesi mbaya kwa Barcelona na Real Madrid watajikuta mmoja wao anaangukia kwenye kundi moja na PSG, Man City au Borussia Dortmund, na Napoli.

Hivi ndivyo timu zilivyogawanywa kwenye makundi na zimepangwa kwa kutegemea kile walichokifanya kwenye mashindano ya Ulaya katika kipindi cha miaka mitano.

Pot One: Bayern Munich, Barcelona, Chelsea, Real Madrid, Manchester United, Arsenal, FC Porto, Benfica.
Pot Two: Atletico Madrid, Shakhtar Donetsk, AC Milan, Schalke, Marseille, CSKA Moscow, PSG, Juventus
Pot Three: Zenit, Man City, Ajax, Borussia Dortmund, Basel, Olympiakos, Galatasaray, Leverkusen
Pot Four: FC Copenhagen, Napoli, Anderlecht, Celtic, Steaua Bucuresti, Viktoria Plzen, Real Sociedad, Austria Vienna

Barcelona taji la 11 na rekodi juu

Barcelona imeshinda taji lake la 11 la Spanish Super Cup na kuweka rekodi katika mchezo uliomalizika kwa suluhu ya bila kufungana dhidi ya Atletico Madrid huku Lionel Messi akikosa mkwaju wa penati.

Timu hizo katika mchezo wa kwanza walimaliza kwa sare ya kufungana bao 1-1 bao la Barcelona likifungwa na Neymar na lile la Atletico Madrid likifungwa na David Villa.

Ubingwa huo ni wa kwanza kwa kocha mpya wa Barcelona Gerardo Martino Tata.

Suarez kuikabili Manchester United



Mchezaji wa liverpool anayetumikia adhabu ya kufungiwa mechi 10 Luis Suarez anaweza kurejea dimbani kuikabili Manchester United wakati timu hizo zitakapokutana kwenye Capital One Cup.

Suarez alipewa adhabu ya kufungiwa mechi 10 baada ya kumngáta beki wa Chelsea Branislav Ivanovic mwezi April na tayari kwenye msimu uliopita amekosa mechi 4.


Lakini Suarez ataukosa mchezo wa Jumapili hii kati ya timu hizo utakaochezwa Anfield.

Ratiba ya mechi za Capital One zitakazochezwa September 24/25


Manchester United v Liverpool
Sunderland v Peterborough
West Ham v Cardiff
Man City v Wigan
Burnley v Nottingham Forest
Newcastle v Leeds
Southampton v Bristol City
West Brom v Arsenal
Swindon v Chelsea
Tranmere v Stoke
Watford v Norwich
Aston Villa v Tottenham
Hull v Huddersfield
Leicester v Derby
Birmingham v Swansea
Fulham v Everton

Wednesday, August 28, 2013

UHUNI : Yanga waipopoa mawe Coastal Union

Hasira za Yanga kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Wagosi wa Kaya Coastal Union zimeishia kwenye basi la Wagosi hao wa Kaya baada ya mashabiki kuamua kulipopoa mawe.

Tukio hilo limetokea nyuma ya uwanja wa Taifa wakati basi lililobeba wachezaji na viongozi wa Coastal Union  lilipokuwa likiondoka uwanjani hapo.

Mashabiki waliokuwa wamebeba mawe walianza kulishambulia basi hilo la Coastal na kupasua vioo ambavyo vimemuuza beki wa pembeni Ahmad Juma aliyechanika sehemu ya nyuma ya kichwa.

Hilo ni tukio la pili mfululizo kwa Coastal Union kushambuliwa na mashabiki wa Yanga,kama itakumbukwa msimu uliopita pia mashabiki wa Yanga waliwahi kuishambulia timu hiyo ya kutokea huko Tanga.

Mkurugenzi wa ufundi wa Coastal Union Nassor Binslum akizungumza na Supermariotz amelaani kitendo hicho akisema si kitendo cha uwanamichezo na kinapaswa kulaaniwa na kila mpenda soka.

Kwenye mchezo huo goli la Yanga limefungwa na Didier Kavumbagu wakati lile la Coastal Union likiwekwa wavuni kwa penati na nahodha Jerry Santo.

Mwamuzi Martin Saanya kutoka Morogoro aliyevurunda katika mchezo huo alitoa kadi nyekundu kwa Crispin Odula wa Coastal Union na Simon Msuva wa Yanga.

Katika michezo mingine iliyochezwa leo Simba wamepata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya JKT Oljoro kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid bao likifungwa na Harun Chanongo.

Huko Tabora kwenye uwanja wa Ally Hassan Mwinyi Azam FC wamechomoza na ushindi wa mabao 2-0 yakifungwa na Gaudance Mwaikimba na Seif Karihe.

Uwanja wa Sokoine Mbeya City wamewafunga maafande wa Ruvu Shooting 2-1 wakati huko Mkwakwani Mgambo JKT wamewachapa Ashanti United 1-0.

Yanga vs Coastal Union live Times fm

Mchezo wa ligi kuu soka Tanzania bara kati ya Yanga na Coastal Union ya Tanga utakaopigwa kwenye uwanja wa Taifa Dar Es Salaam utatangazwa moja kwa moja na kituo cha Radio cha Times fm 100.5 kuanzia saa 10.30 jioni

Kiingilio kwenye mchezo huo itakuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000. Mwamuzi Martin Saanya wa Morogoro ndiye atakayepuliza filimbi wakati Kamishna atakuwa Omari Walii kutoka Arusha.
Mechi nyingine za leo Mtibwa Sugar itaikaribisha Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Manungu ulioko Turiani mkoani Morogoro wakati Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora utakuwa mwenyeji wa pambano kati ya wenyeji Rhino Rangers na Azam.

Vumbi lingine litatimka kwenye Uwanja wa Mabatini ulioko Mlandizi mkoani Pwani wakati maafande wa JKT Ruvu watakapokwaruzana na wenzao wa Tanzania Prisons kutoka Mbeya. Mbeya City na Ruvu Shooting zitacheza kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya. 

Jiji la Tanga litakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Mgambo Shooting na Ashanti United itakayochezwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani. Oljoro JKT itakuwa mwenyeji wa Simba kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Kaluta Amri Abeid jijini Arusha.

Williams atua kumkabili Cheka

Mpinzani wa bondia Francis Cheka kutoka nchini Marekani Phil Williams ametua nchini tayari kwa pambano hilo litakalofanyika Ijumaa August 30 kwenye ukumbi wa Diamond Jubillee.

Pambano hilo ni la kimataifa kuwania ubingwa wa WBF.
Mgeni rasmi katika pambano,Bondia bingwa wa Dunia wa Uzito wa Juu wa  Zamani, Francois Botha 'White Buffalo' (wa pili kushoto) tayari ametua nchini kushuhudia Cheka na Williams wakiusaka mkanda huo.

Tuesday, August 27, 2013

Mpera mpera ligi kuu,Yanga Coastal Union watauana

Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inaingia raundi ya pili kesho (Agosti 24 mwaka huu) kwa timu zote 14 kuwa viwanjani huku macho na masikio ya washabiki wengi yakielekezwa kwenye mechi kati ya Yanga na Coastal Union.

Mechi hiyo itachezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10.30 jioni kwa kiingilio cha sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000. Mwamuzi Martin Saanya wa Morogoro ndiye atakayepuliza filimbi wakati Kamishna atakuwa Omari Walii kutoka Arusha.

Mtibwa Sugar itaikaribisha Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Manungu ulioko Turiani mkoani Morogoro wakati Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora utakuwa mwenyeji wa pambano kati ya wenyeji Rhino Rangers na Azam.
Vumbi lingine litatimka kwenye Uwanja wa Mabatini ulioko Mlandizi mkoani Pwani wakati maafande wa JKT Ruvu watakapokwaruzana na wenzao wa Tanzania Prisons kutoka Mbeya. Mbeya City na Ruvu Shooting zitacheza kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.
Jiji la Tanga litakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Mgambo Shooting na Ashanti United itakayochezwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani. Oljoro JKT itakuwa mwenyeji wa Simba kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Kaluta Amri Abeid jijini Arusha.

Mourinho ampa Rooney saa 48


Kocha Jose Mourinho amempa saa 48 mshambuliaji Wayne Rooney kuamua kama anaondoka au anabaki Manchester United au anatua Stamford Bridge.

Mourinho amemtaka Rooney kuomba kuondoka na aliweke suala hilo hadharani watu waelewe anachotaka.
United tayari wamesema mshambuliaji huyo hauzwi na alikuwemo kwenye kikosi kilicholazimishwa sare ya bila kufungana na Chelsea.

Mourinho tayari ametumbukiza ofa mbili ambazo zimechomolewa na Manchester United ili kumnasa nyota huyo ambaye katika mchezo wa jana alipokelewa vizuri na mashabiki wa klabu hiyo.
Alipoulizwa Mourinho kama atapeleka ofa ya tatu kama alivyoahidi kabla ya mchezo wa jana akasema Manchester United inaweza kuwa klabu ya kipekee,kwasababu klabu yoyote duniani ambayo mchezaji anataka kuhama hawawezi kumuunga mkono watampa wakati mgumu lakini imekuwa tofauti kwa United ambao wamemuunga mkono kwa asilimia zote kwenye mchezo wa jana.

Mourinho akasema amesema watakuwa wa kwanza kuheshimu kile atakachoamua Rooney.

Chelsea tayari wana chaguo lingine,ikielezwa kuwa rada zao zimemnasa mshambuliaji wa Anzhi Makhachkala MCameroon Samuel Eto'o na ndio maana wametoa saa 48 kwa Rooney ili wapate muda wa kusema na Etoo.
Wakati huo huo Rooney hana mpango wa kulazimisha kuondoka kwa kuwasilisha maombi ya kuondoka kimaandishi.
Licha ya mshambuliaji huyo kutotaka kulazimisha kuondoka inaelezwa bado mambo yake hayajapatiwa ufumbuzi.

Bale aipasua kichwa Spurs



Mshambuliaji wa Tottenham Gareth Bale ameshindwa kutokea kwenye mazoezi ya timu hiyo aliyotakiwa kuripoti leo akitokea Marbella.

Bale, 24,anatajwa kuwa karibu kuweka rekodi ya dunia ya dau la paundi milioni 86 kutoka kwa Real Madrid lakini Spurs wamesema hakuna makubaliano yaliyofikiwa.
 
Tottenham imepokea offer nyingine nje ya Real Madrid japo bado haijatajwa lakini inaelezwa kuwa ni Manchester United.

Spurs walimtaka Bale kuripoti leo Jumanne lakini hakuna sababu zozote zilizotolewa za kushindwa kutokea.
Inaaminika kuwa huko Hispania Real Madrid wametengena stage iliyopewa jina la 'Bale Box', ambayo imewekwa kwenye uwanja wao wa Santiago Bernabeu itakayotumika kumtambulisha kwa mashabiki wa klabu hiyo.