Friday, August 9, 2013
Macho yote kwa PSG na Monaco
Macho yote yatakuwa kwa mabingwa watetezi Paris Saint-Germain na matajiri wa Monaco wakati ligi kuu ya Ufaransa Le Championate itakapoanza kuunguruma wikiendi hii.
Kocha mpya wa PSG Laurent Blanc ameweka wazi kuwa kushindwa kunyakuwa taji ni kufeli kwa timu hiyo ghali.
Mchezo wa kwanza wa Blanc ni dhidi ya Montpellier leo wakati Monaco waliorejea ligi kuu wanaanza kibarua chao dhidi ya Bordeaux kesho.
PSG wametumia kitita kikubwa kwa mara nyingine kwenye soko la uhamisho wa wachezaji wakimnasa mshambuliaji wa Uruguay Edinson Cavani kwa dau la Euro milioni 64 kutokea Napoli.
Branc anasema lengo lao litakuwa halijatimia kama watamaliza kwenye nafasi ya pili kwakuwa lengo lao ni kufanya vizuri kwa kadiri wanavyoweza kwenye mashindano yote ambayo wanashiriki.
PSG wanaelezewa kuwa na safu kali ya ushambuliaji inayoongozwa na Cavani na Zlatan Ibrahimovic Ibra Cadabra.
Monaco naoa wametumia fedha nyingi kuimarisha kikosi chao wakimnasa Radamel Falcao kutokea Atletico Madrid kwa dau la Euro milioni 60,pia wakiwanasa Joao Moutinho na James Rodriguez kutoka Porto, Eric Abidal, Jeremy Toulalan na Ricardo Carvalho.
Mechi nyingine za kesho Jumamosi :
Evian v Sochaux
Lille v Lorient
Valenciennes v Toulouse
Lyon v Nice
Rennes v Reims.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.