Tuesday, August 20, 2013
Man City yamsikilizia Kompany
Manchester City wanasubiri ili kujua nahodha wake Vincent Kompany atakaa nje kwa muda gani baada ya kuumia kwenye mchezo wa hapo jana usiku dhidi ya Newcastle United.
Beki huyo raia wa Ubelgiji aliumia wakati Manchester City ikiichapa Newcastle kwa mabao 4-0 na sasa klabu hiyo inabaki na pengo kubwa kwenye ukuta wake baada ya kuumia kwa Micah Richards,huku beki pekee wa katikati ambaye si majeruhi ni Joleon Lescott.
Kocha Manuel Pellegrini amesema hawezi kusema lolote kuhusiana na beki huyo mpaka atakapopata taarifa sahihi ya madaktari lakini kwa mtazamo wa haraka anaona inawezekana akakaa nje kwa wiki moja au mbili.
Kwa tatizo hilo la beki wa kati linaweza kumsukuma Pellegrini kuingia sokoni ili kusaka beki wa kati ikiwa pia tayari bila ya beki wake mpya Matija Nastasic,ambaye ana maumivu ya kifundo cha mguu alichoumia wakati wa maandalizi ya kabla ya msimu kwenye Barclays Asia Trophy japo tayari MSerbia huyo amerejea kwenye mazoezi.
Pamoja na majanga hayo kikosi hicho cha Pellegrini jana kilianza vizuri ligi kuu ya England kwa mabao ya David Silva, Sergio Aguero, Yaya Toure na Samir Nasri.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.