Kocha wa timu ya taifa ya England Roy Hodgson amesema mshambuliaji Wayne Rooney si majeruhi baada ya kumuona akishughulika ipasavyo kwenye mazoezi ya jana.
Mshambuliaji huyo wa Manchester United, 27, hakushiriki kwa asilimia 100 kwenye maandalizi ya kabla ya msimu na klabu yake ya Manchester akidaiwa kuumia bega na hakuwemo kwenye kikosi kilichoichapa Wigan kwa mabao 2-0 kwenye Community
Shield Jumapili.
Rooney alifika mapema kwenye mazoezi na akamaliza pasipo rabsha yoyote kwenye maungo yake na alipoulizwa Hodgson
amesema ni ngumu kuona uwezo wa mtu kucheza au kutocheza kwa sababu ya maumivu kwa kutumia macho ya kawaida lakini anaamini mshambuliaji huyo hana maumivu yoyote.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.