Thursday, August 1, 2013

Simba yaunga mkono mechi za ligi kuu kuwa live Azam Tv

Wekundu wa Msimbazi Simba wameunga mkono mechi za ligi kuu soka Tanzania bara kuanzia msimu ujao kuoneshwa live na Azam Media kupitia kituo chake cha Televisheni cha Azam Tv.

Afisa habari wa Simba Ezekiel Kamwaga amesema kuna faida kubwa mechi kuonekana moja kwa moja kwenye Televisheni kwahiyo wao kwa upande wao hawana sababu ya kukataa hilo lakini pia wakisema wanaamini linapokuja suala la kucheza uwanjani timu zote zipo sawa.
Mahasimu wa Simba kwenye soka la Tanzania Yanga Africa wenyewe wameweka ngumu mechi zao kuoneshwa live na Azam Tv wakisema wanataka kulipwa zaidi ya timu nyingine,lakini pia wakitia ngumu kwasababu Azam FC ni wapinzani wao wakubwa kwenye soka la Tanzania.

Azam Media wameingia mkataba wa awali wa kuonesha mechi za ligi kuu ya VodaCom kwa miaka mitatu wakimwaga kiasi cha shilingi bilioni 5.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.