Monday, August 19, 2013
Mourinho asema atapigana mpaka siku ya mwisho
Jose Mourinho ameweka wazi kiu yake ya kutaka kusajili mshambuliaji kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili huku Wayne Rooney akionekana kuwa zaidi katika rada za kocha huyo.
The Blues tayari wamepeleka ofa mbili ambazo zimechomolewa na Manchester United.
Meneja wa United David Moyes ameendelea kushikilia msimamo wa kwamba mshambuliaji huyo hauzwi na yupo kwenye mipango yake.
Mourinho anataka kurudi na ofa ya tatu kabla ya kufungwa kwa usajili kwakuwa anataka kuongeza changamoto ya kutumbukiza mabao kwenye safu yake ya ushambuliaji.
Anasema watajaribu mpaka siku ya mwisho na mambo yao wanafanya kiofisi na hawana tabia kama ya baadhi ya vilabu ambavyo vinazungumza na mchezaji na kumshinikiza aombe kuondoka.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.