Monday, August 26, 2013

Mourinho ambebesha zigo Moyes


Kocha wa Chelsea Jose Mourinho anaamini kocha wa Manchester United David Moyes anatakiwa kubeba lawama kwa sakata la usajili linalohusiana na mshambuliaji Wayne Rooney.

Mourinho,amezungumza hayo alipokuwa akijibu swali linalohusiana na uhamisho wa Rooney na jinsi atakavyopokewa na mashabiki wa United wakati wa mchezo wao wa leo wa ligi kuu ya England utakaopigwa Old Trafford.
Kocha huyo anashangaa yeye kulaumiwa akisema analaumiwa kwa lipi wakati sio yeye aliyesema Rooney atakuwa chaguo la pili,anachojaribu kufanya ni kumsajili mchezaji ambaye kocha wake amemtaja kama chaguo la pili na hawakutaka kumsajili Robin Van Persie ambaye ni chaguo la kwanza.

Anasema yeye si wa kulaumiwa akitolea mfano wa katika timu yake kama akisema Ramires ni chaguo la pili na atacheza kama Frank Lampard ataumia na ikajitokeza timu ikataka kumnunua hakuna atakayemshambulia na kumlaumu aliyejitokeza kumnunua.

Mourinho hakuficha kusema kuwa mtu wa kubeba zigo la lawama ni Moyes aliyetamka hadharani kuwa Rooney si chaguo lake la kwanza.
Anasema kila timu kubwa huwa na chaguo la pili ambalo pia ni bora lakini pointi yake ni kwamba kama mchezaji husika anakubaliana na hilo hakuna tatizo lakini kama hakubaliani nalo hilo ni jambo lingine.

Timu hizo zinakutana leo kwenye ligi kuu ya England na kocha wa Manchester United David Moyes ataamua kama amjumuishe kikosini Rooney kwenye wachezaji 11 watakaoanza katika mchezo dhidi ya timu inayojaribu kumsajili.
Katika mchezo huo Rafael yupo nje kwa mwezi mmoja,Nani,Ashley Young na Javier Hernandez wote ni majeruhi.

Kwa Chelsea beki raia wa Brazil David Luiz anaweza kuwa nje kwakuwa ni majeruhi lakini Mourinho anaweza pia kuchukua uamuzi wa kumuanzisha mshambuliaji Romelu Lukaku katika sehemu ya ushambuliaji.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.