Thursday, August 8, 2013

Suarez apigwa benchi mazoezini,sasa ni jino kwa jino na Brendan Rodgers

Mshambuliaji wa Liverpool Luis Suarez amepigwa benchi na sasa ameambiwa afanye mazoezi ya peke yake na kocha Brendan Rodgers,ambaye amesema mshambuliaji huyo ameikosea heshima klabu hiyo.

Rodgers akiwa na hasira amekanusha kutoa ahadi ya kumruhusu mshambuliaji huyo kuhamia timu nyingine kama Liverpool itakosa nafasi ya kucheza ligi ya mabingwa barani Ulaya.


Kocha huyo anasema hakuna ahadi iliyotolewa na hakuna ahadi ambayo imevunjwa kama Suarez anavyodai.
 
Mshambuliaji huyo raia wa Uruguay amelipeleka hadharani jambo hilo akiamini kuwa Liverpool wamekiuka kipengele katika mkataba kwa kukataa kumuuza na ameachwa huko Merseyside akitakiwa kufanya mazoezi peke yake wakati klabu hiyo yenyewe ikiwa Norway ilikocheza na Valerenga na kuichapa mabao 4-1.

 Suarez, 26,amepanga kuwasilisha maombi ya uhamisho wiki hii kama klabu hiyo itaendelea kushikilia msimamo wa kutomuuza.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.