Shirikisho la soka la dunia Fifa limeilima faini shirikisho la soka la Brazil kwa kushindwa kuwasilisha mapema taarifa za vipimo vya dawa zisizoruhusiwa michezoni.
Fifa imesema imeilima faini Brazil ya Swiss francs 10000 sawa na dola 10 700 takribani shilingi milioni 17 za kibongo kwa kushindwa kufuata matakwa ya kamati ya nidhamu ya shirikisho hilo,wakishindwa kuwasilisha taarifa hizo kwa wakati.
Shirikisho hilo halijaweka wazi jina la mchezaji husika lakini vyombo vya habari vya Brazil vinadai kuwa ni mchezaji wa zamani wa Vasco da Gama Carlos Alberto,ambaye tayari amesafishwa na tuhuma hizo baada ya majibu kuonesha kuwa yuko sawa.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.