Wednesday, August 7, 2013

Mkataba wa Kaseja Lupopo wa Kifaransa


Nahodha na golikipa namba moja wa timu ya Taifa ya Tanzania Juma Kaseja ameshindwa kusaini mkataba na timu ya FC Lupopo ya Congo DRC baada ya mkataba kuletwa kwa lugha ya Kifaransa.

Kaseja alikubaliana kila kitu na Lupopo ikiwa pamoja na yale aliyotaka yawekwe kwenye mkataba kabla ya kusaini na kwenda kuitumikia klabu hiyo.
Lupopo wametuma mkataba huo leo lakini imeshindikana kusainiwa kwakuwa upo kwenye lugha ambayo Kaseja ameomba ibadilishwe na kuwekwa kwenye lugha ya Kiingereza ili aone kama alichoomba ndicho kilichoandikwa.

Mkataba huo sasa huenda ukasainiwa kesho kama utakuwa umebadilishwa na Kaseja kuridhika na kile kilichomo ndani ya mkataba.

Kaseja amemaliza mkataba na Simba ambao viongozi wake waliweka wazi kuwa hawataongeza mkataba mwingine na golikipa huyo aliyedumu zaidi ya miaka 10 kwenye klabu hiyo.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.