Wednesday, August 14, 2013

BREAKING NEWZ : Vigogo wakutana Wizarani kuijadili Yanga kuikataa Azam Media

Vigogo mbalimbali wa soka wanakutana muda huu Wizara ya habari,vijana,utamaduni na michezo kujadili sakata la klabu ya Yanga kukataa haki za kuoneshwa kwa ligi kuu ya Tanzania bara kupewa Azam Media.
Vigogo hao kutoka timu mbalimbali,shirikisho la soka nchini TFF,Azam Media,kamati ya ligi na serikalini wanakutana kujadili kwa kina na huenda wakatoka na muafaka.

Vigogo wanaohudhuria kikao hicho ambao mpaka sasa wamekwishaingia ndani ya ofisi za wizara hiyo ni pamoja na mjumbe wa kamati ya ligi Geofrey Iric Nyange Kaburu,Rais wa TFF Leodger Tenga,katibu mkuu wa TFF Angetile Osiah,makamu mwenyekiti wa Yanga Clement Sanga na katibu mkuu wa Yanga Lawrance Mwalusako.

Wengine waliowasili kwenye kikao hicho ni mkurugenzi wa ufundi wa Cioastal Union Nassor Binslum,mkurugenzi wa michezo Leonard Thadeo na mkurugenzi msaidizi wa maendeleo ya michezo Juliana Matagi Yasoda.
Mwenyeji wa mkutano huo ni naibu waziri wa habari vijana utamaduni na michezo Amos Makalla.


No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.