Kucheza ama kutocheza kwa mshambuliaji Mrisho Khalfan Ngassa Anko kwenye ligi kuu soka Tanzania lipo mikononi mwa Yanga baada ya Wekundu wa Msimbazi Simba kusema hawana sababu ya kumngángánia mshambuliaji huyo wanachotaka ni kulipwa chao.
Afisa habari wa Simba Ezekiel Kamwaga amesema kwasasa hawana shida na Ngassa kinachotakiwa ni Yanga kuwalipa chao ili waweze kumtumia baada ya kumalizika kwa adhabu yake ya kufungiwa mechi sita.
Kamwaga amesema hawana shaka yoyote na maamuzi yaliyofanywa na kamati ya sheria, maadili na hadhi za wachezaji chini ya mwenyekiti wake Alex Mgongolwa.
Amesema walikuwa wanamngángánia Ngassa kwakuwa walikuwa wanafahamu walimsainjisha mkataba na walichotaka ni kujua hatima ya fedha yao waliyompa suala ambalo kamati imelitatua na sasa hawahitaji huduma ya mchezaji huyo zaidi ya kupewa fedha yao.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.