Wednesday, August 7, 2013
Suarez bado hakieleweki kwa Liverpool
Luis Suarez amesema anajiandaa kulipeleka suala lake kwenye kamati ya ligi kulazimisha kuondoka kwenye klabu ya Liverpool.
Mshambuliaji huyo alitakiwa mara mbili na Arsenal ambao dau lao lilipigwa chini kitu anachodai kuwa klabu hiyo imekiuka makubaliano ya awali.
Suarez amesitisha mpango wake wa kuwasilisha maombi ya maandishi ya kutaka kuondoka na ameripoti kwenye mazoezi ya klabu hiyo yaliyofanyika leo lakini amesisitiza kuwa bado ataendelea kushinikiza kuondoka kwake.
Arsenal imebaki kuwa klabu pekee ambayo imewasilisha ofa ya kumtaka Suarez kwa dau la paundi milioni 41.
Suarez amesema mwaka uliopita alikuwa na nafasi ya kutakiwa kwenye moja ya timu kubwa Ulaya lakini akabakia kwenye timu hiyo kwa makubaaliano ya kwamba kama Liverpool watashindwa kufuzu kucheza ligi ya mabingwa ataruhusiwa kuondoka kitu ambacho hakijafanyika.
Anasema anaaona kuwa klabu hiyo imemsaliti na imekwenda kinyume na mkataba ambao si tu ulifanyika kwa mdomo bali pia ulikuwa kimaandishi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.