Hatima ya mshambuliaji Cristiano Ronaldo ndani ya Real Madrid
bado tata haieleweki baada ya kukataa kuthibitisha taarifa za kwamba amekubali kuongeza mkataba mwingine wa miaka mitano na klabu hiyo.
Mkataba wa sasa wa Ronaldo ndani ya Madrid umebakiza miaka miwili kumalizika na alitua kwenye klabu hiyo akitokea Manchester United kwa dau linaloshikilia rekodi ya dunia la paundi milioni 80 mwaka 2009.
Ronaldo amesema hawezi kuthibitisha lolote na anafanya kazi kama anvyofanya siku zote na kuhusua hatima yake ya mbele anasema hajui lolote kwasasa yeye ni mchezaji wa Real Madrid.
Madrid wapo kwenye ziara huko Los Angeles nchini Marekani ambako Jumatano wanatarajia kucheza na Chelsea kwenye mchezo wa fainali baada ya kuwachapa Everton huku Chelsea wakiichapa AC Milan.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.