Friday, August 16, 2013
Chelsea wahesabu siku kumtosa Rooney
CHELSEA wanataka kukamilisha usajili wa Wayne Rooney kufikia August 26 ikishindakana watanyoosha mikono.
Bosi wa The Blues Jose Mourinho anamuhitaji Rooney kwenye klabu hiyo wakati ambapo wanawafuata Manchester United huko Old Trafford.
Tayari ofa mbili za klabu hiyo zimekataliwa na wiki hii wanataka kupeleka ofa ya mwisho kumnasa Rooney ambaye anataka kuondoka huku klabu yake ikisema hauzwi kwa dau lolote.
Kocha wa Manchester United David Moyes amesema hakuna lolote jipya kwasasa kuhusu Rooney na kila mmoja wamemwambia mshambuliaji huyo hauzwi japo anakiri kuwa amechoshwa na sakata hilo.
Chelsea wanafikiria kunyoosha mikono kwa mshambuliaji huyo na Mourinho anageukia kwa mshambuliaji wa Anzhi Makhachkala Samuel Eto’o kwa dau la paundi milioni 5 na tayari yupo hatua chache kuinasa saini ya mkali huyo kutoka Cameroon.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.