Monday, August 26, 2013

Man City yazamishwa na Cardiff,Pellegrini alalama kona zimewaua


Boss wa Manchester City Manuel Pellegrini amelaumu uwezo wao finyu wa kucheza mipira ya kona ambao umepelekea kipigo cha kushtua cha mabao 3-2 kutoka kwa wageni wa ligi kuu ya England EPL Cardiff City.

Pellegrini anasema kona ndiyo imeamua mchezo wa jana ambao hawakucheza vizuri japo akasema pia ilikuwa ngumu kwao kuifunga Cardiff kwakuwa walikuwa wanacheza wachezaji 10 karibu na eneo la lango lao wakijaribu kujilinda zaidi.

Udhaifu huo hata hivyo haukumfanya Pellegrini kujilaumu kuwakosa mabeki wake wa kati Vincent Kompany na Matija Nastasic.
Edin Dzeko alingárisha nyota yake kwenye mchezo huo akitupia wavuni lakini Aron Gunnarsson akaisawazishia Cardiff na baadaye mabao mawili yaliyofungwa kwa kichwa na Fraizer Campbell yakawazamisha Manchester City.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.