Friday, August 23, 2013

Anelka anaacha soka



Mshambuliaji Nicolas Anelka amewaambia West Brom kuwa anaweza akaachana na soka baada ya kufariki wakala wake Eric Manasse lakini kocha Steve Clarke ana matumaini kuwa mshambuliaji huyo atarejea mzigoni.

Mshambuliaji huyo ambaye amesajiliwa kwenye usajili unaoendelea wa majira ya joto atakuwa nje kwa mchezo wa kesho Jumamosi dhidi ya Everton kwakuwa yupo kwenye mapumziko hayo ya maombolezo.
Clarke alipoulizwa kama Anelka amesema ataachana na soka akasema mchezaji huyo amesema maneno hayo lakini bado wanampa muda wa kwenda kufukiria.

Kocha huyo amesema Anelka aliyecheza mechi 69 kwa timu ya Taifa ya Ufaransa aliondoka mazoezini Alhamis baada ya kuzungumza naye pamoja na mkurugenzi wa ufundi Richard Garlick.

Anelka ametwaa mataji ya ligi kuu ya Uingereza akiwa na Arsenal,Chelsea,lakini pia amechezea Liverpool, Manchester City na Bolton.

Ameshinda Uefa Champions League mwaka 2000 akiwa na Real Madrid.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.