Friday, August 23, 2013

UMAFIA : Chelsea yamteka Willian kwa Spurs


Jose Mourinho na Chelsea wamefanya umafia na kuiteka dili ya kumsajili kiungo mshambauliaji wa Anzhi Makhachkala Willian mwenye thamani ya paundi milioni 30.

Mourinho amesema kuwa kiungo huyo ameaichagua Chelsea badala ya Tottenham.
 
Willian, 25, almefanyiwa vipimo vya afya na Spurs,lakini sasa anaweza kusaini kuichea Chelsea baada ya timu hiyo kuingilia kati jana.

Alipoulizwa kama MBrazil huyo amechagua kwenda Stamford Bridge, Mourinho akatikisa kichwa kukubaliana na hilo akisema anajua nini mchezaji huyo anakitaka na kwa hatua iliyofikia sasa hawawezi kuficha kuna uwezekano wa kumsajili mchezaji huyo.
Willian alijiunga na Anzhi mwezi January kwa dau la paundi milioni 30 akitokea Shakhtar Donetsk ya Ukraine.

Mmiliki wa Chelsea Roman Abramovich ameingilia mpango wa Spurs baada ya kuwasiliana moja kwa moja na Anzhi kutoa ofa kama waliyotoa Spurs.
Willian amevutiwa na mpango wa kucheza kwenye champions league,kupigania taji la ligi kuu na kucheza chini ya Mourinho.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.