Monday, May 26, 2014

Chelsea yatumbukia kwa Lavezzi,PSG wawataka Oscar,Hazard na Cech


Chelsea wametumbukia kumtaka mshambuliaji wa Paris St Germain Ezequiel Lavezzi.

Klabu hiyo ya Ufaransa imemsaini beki David Luiz na inaonesha nia ya kuwataka Eden Hazard, Oscar na Petr Cech.
Inafahamika kuwa Chelsea nao wameulizia bei ya Lavezzi ambaye ana kiu ya kucheza kwenye ligi ya kiushindani Zaidi.

Chelsea wanatazama kuimarisha safu yake ya ushambuliaji Samuel Eto'o amemaliza mkataba wake huku pia ikiwa tayari imekubaliana na Atletico Madrid kumsajili mshambuliaji wake Diego Costa.
Jose Mourinho pia anataka kuwapora Manchester City beki Eliaquim Mangala kutokea FC Porto ambaye yupo karibu kutua City huku pia ikimtaka Raphael Varane wa Real Madrid.
 

Tuesday, May 20, 2014

Msimu mpya ligi kuu August 24,usajili kufunguliwa rasmi June 15

Usajili wa wachezaji kwa hatua ya kwanza msimu huu 2014/2015 unaanza Juni 15 hadi Agosti 3 mwaka huu wakati kipindi cha kutangaza wachezaji walioachwa au kusitishiwa mikataba ni kuanzia Juni 15-30 mwaka huu.

Kipindi cha kwanza cha uhamisho wa wachezaji ni kuanzia Juni 15 mwaka huu hadi Julai 30 mwaka huu,Kupitia majina na kutangaza pingamizi ni kati ya Agosti 4 na 11 mwaka huu,Kuthibitisha usajili hatua ya awali ni Agosti 12 hadi 14 mwaka huu.

Usajili hatua ya pili utakuwa kati ya Agosti 14 na 29 mwaka huu,Kupitia na kutangaza majina ya pingamizi hatua ya pili ya usajili ni kuanzia Agosti 30 hadi Septemba 4 mwaka huu,Uthibitisho wa usajili hatua ya pili ni Septemba 5 na 6 mwaka huu.

Kwa upande wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inatarajiwa kuanza Agosti 24 mwaka huu, na ratiba inatarajiwa kutoka mwezi mmoja kabla (Julai 24 mwaka huu).

Chokoraa aweka muziki pembeni ageukia masumbwi,kushuka ulingoni May 24

Mwanamuziki na kiongozi wa bendi ya Mapacha watatu Khalid chokoraa anategemea kupanda ulingoni Jumamosi May 24 katika ukumbi wa friends corner kuzipiga na bondia chipukizi Abdul Manyenza.

Chokoraa amesema muda mrefu amekuwa akifanya mazoezi ya kujenga mwili na ya ngumi huku akipigana na mabondia mbalimbali mazoezini kiasi cha kujiona ana uwezo wa kupanda ulingoni.

Amesema sasa ni nafasi ya kuonesha kipaji kingine mbali na muziki.

Mandzukic,Guardiola kimenuka


Mario Mandzukic anaelekea kucheza soka huko England,na anaweza kuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na kocha mpya wa Manchester United Louis Van Gaal baada ya kubwatukiana na kocha wa Bayern Munich Pep Guardiola.

Arsenal na Chelsea wanaongoza katika mbio za kumnasa mshambuliaji huyo mwenye miaka 27 kapo United nao wanataka kutumbukia katika mbio za kumnasa.

Mandzukic anaondoka kwa mabingwa hao wa Bundesliga akielezea wazi kutoridhishwa na muelekeo wa na mbinu za Guardiola na tayari kocha huyo amemtakia kila la kheri kusaka maisha mapya kwenye klabu nyingine.

Guardiola hakumuweka kikosini mchezaji huyo kwenye mchezo uliopita walioichapa Borussia Dortmund 2-0 Jumamosi iliyopita katika kombe la Ujerumani licha ya kuwa hakuwa mgonjwa.

Kocha huyo baada ya kujihakikishia kikosi ambacho kingecheza mchezo huo siku ya Alhamis alimfuata Mandzukic,na kumwambia amemtema kwenye kikosi kitakachocheza mchezo huo na akamtakia kila la kheri na klabu yake mpya.

Monday, May 19, 2014

Kamati ya uchaguzi Simba yarudisha wagombea wote,pingamizi kuanza rasmi kesho,watatu wapigwa panga kamati ya uchaguzi


Kamati ya uchaguzi ya wekundu wa msimbazi Simba, imetangaza majina ya awali ya wagombea 40 waliotimiza masharti yaliyowekwa katika fomu za kuwania nafasi mbalimbali za uongozi wa klabu hiyo utakaofanyika mwishoni mwa mwezi ujao

Akitangaza majina hayo mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya Simba Damas Ndumbaro amesema wagombea wote waliochukua na kurejesha fomu wamepitishwa kwenye hatua ya awali na kuanzia kesho wanachama ruksa kuanza kuwawekea pingamizi ikifuatiwa na usaili.

Aidha kamati hiyo imelaani kitendo cha wagombea kusindikizwa na kundi la wanachama na vikundi vya ngoma wakati wa zoezi la uchukuaji na urudishaji fomu jambo ambalo linaashiria kuanza kwa kampeni za chini kwa chini.

Ndumbaro amesema kamati yake itakapojiridhisha kutokea tena kwa tukio kama hilo, watawajibika kuchukua hatua kali zaidi za kumuengua mgombea kunako kinyang’anyiro hicho.

Pamoja na mambo mengine Ndumbaro akafafanua ni kwanini wamewapitisha wagombea wote waliochukua fomu na kurejesha fomu wakati wapo wanachama waliobainika kukosa sifa na vigezo vya kugombea.

Inaelezwa kuwa baadhi ya wagombea hawana vyeti vya elimu ya sekondari lakini wapo ambao wanatajwa kuwa bado wanatumikia vifungo mbalimbali licha ya kuwepo upotoshwaji kuwa wagombea hao wamesafishwa kwa masamaha wa Rais wa TFF.

Kama itakumbukwa wakati Rais wa TFF Jamal Emily Malinzi anatangazwa kuwa rais mpya wa shirikisho la mpira wa miguu nchini Octoba 28 mwaka jana, alitangaza kuwasamehe waliokuwa wakikabiliwana na vifungo mbalimbali isipokuwa wale wenye kesi za kula rushwa, kutoa rushwa na kupanga matokeo.

Aidha katika msamaha huo akatanabahisha kuwa hauhusiani na msamaha wa vilabu kwasababu vilabu vina taratibu zake.

Wakati huo huo kamati ya utendaji ya wekundu wa msimbazi Simba imefanya mabadiliko ya kamati yake ya uchaguzi kwa kumuongeza mjumbe mmoja mwanasheria Evodius Mmanda na kuwaengua wengine watatu akiwemo Kassim Dewji na Juma Simba Gadafi.