Kutinga hatua ya fainali ya kombe la FA inaweza ikawa ushindi tosha kwa Hull City hata kama watapoteza na kukosa taji hilo hapo kesho ndani ya Wembley.
Timu hiyo imeonesha kumshukuru kocha wao Steve Bruce kwa kuwaweka kwenye kilele cha mafanikio katika msimu huu na wameamua kutengeneza mifuniko ya choo ambayo ina rangi za timu hiyo na picha ya Bruce.
Hiyo ina maana kocha huyo anabaki kwenye kumbukumbu muhimu za timu hiyo na mashabiki kila wanapoingia chooni wanakutana na taswira ya kocha wao wa mafanikio.
Choo kikifunikwa kinakuwa na rangi za timu hiyo na kikifunuliwa unakutana na picha ya Bruce.
Hata kama watafungwa kwenye fainali hiyo mashabiki wa Hull City bado watasheherekea mafanikio kwa kucheza fainali yao ya kwanza ya FA.
Sehemu ya juu ya choo kikifunikwa |
Sehemu ya ndani ya choo kikifunuliwa mfuniko |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.