Friday, December 27, 2013

Chelsea kumtoa sadaka Demba Ba


Chelsea wako tayari kumtoa sadaka mshambuliaji wake Demba Ba ili kumnasa Fredy Guarin kutoka Inter Milan ya Italia.

The Blues wako tayari kukaa na Inter Milan ili kumnasa kinda huyo wakati wa usajili wa dirisha dogo katika harakati za kutaka kujiimarisha hasa katika safu ya ushambuliaji inayoonekana kutokaa sawa.

Inaelezwa kuwa inaweza kuwaghalimu Chelsea kitita cha paundi milioni 16 ili kumnasa kinda huyo wa Colombia ambaye amewahi kucheza FC Porto.

Walter Mazzarri bosi wa Inter Milan hata hivyo ana shaka kama Ba ataweza kuwa mtu sahihi kwenye kikosi chake.

Chelsea are willing to offer Demba Ba to Inter Milan as a makeweight in their bid to sign Fredy Guarin.
The Blues are already locked in negotiations with the Serie A side over a deal to sign the Colombia midfielder.
However, the two clubs are still yet to agree a fee, with Inter unwilling to lower their £16.5m valuation of the former Porto man.
Ba, who has scored only three league goals since his January switch to Stamford Bridge, is reportedly expendable at west London and Chelsea are willing to offer the Senegal striker and cash to the San Siro club in return for Guarin.
But despite Inter’s need for attacking reinforcements, Calciomercatonews claim Inter boss Walter Mazzarri is unsure of Ba’s suitability for his side.

Read more at http://talksport.com/football/chelsea-ready-use-ba-makeweight-deal-inter-milan-star-13122473047#zxq1kTjSYPM8zzpS.99
Chelsea are willing to offer Demba Ba to Inter Milan as a makeweight in their bid to sign Fredy Guarin.
The Blues are already locked in negotiations with the Serie A side over a deal to sign the Colombia midfielder.
However, the two clubs are still yet to agree a fee, with Inter unwilling to lower their £16.5m valuation of the former Porto man.
Ba, who has scored only three league goals since his January switch to Stamford Bridge, is reportedly expendable at west London and Chelsea are willing to offer the Senegal striker and cash to the San Siro club in return for Guarin.
But despite Inter’s need for attacking reinforcements, Calciomercatonews claim Inter boss Walter Mazzarri is unsure of Ba’s suitability for his side.

Read more at http://talksport.com/football/chelsea-ready-use-ba-makeweight-deal-inter-milan-star-13122473047#zxq1kTjSYPM8zzpS.99

Tuesday, December 24, 2013

EXCLUSIVE : Sina bifu na Ivo-Kaseja


GOLIKIPA wa Yanga Africa aliyewahi kucheza Simba Juma Kaseja amefunguka kuhusu suala la kutompa mkono golikipa wa Simba aliyewahi kucheza Yanga Ivo Mapunda.

Kaseja amesema tofauti na watu wanavyofikiri lakini yeye kwa upande wake hana bifu lolote wala chuki na Ivo na kwake ilikuwa kitu cha kawaida.

"Unajua kaka watu wanaongea sana lakini mimi sina bifu lolote na Ivo,hivyo ni vitu vya kawaida tu na maamuzi ya mtu" alisema Kaseja.

Amesema kuwa hakuwa na sababu yoyote ya kutompa mkono Ivo zaidi ya kuamua kufanya hivyo kwasababu yale ni maamuzi yake binafsi na si sababu ya bifu au chuki baina yao.

Kaseja si mchezaji wa kwanza kutopeana mikono na mchezaji mwenzake au kiongozi wakati wa kusalimiana kabla ya kuanza kwa mchezo,imewahi kutokea kwa Steven Mapunda na Mohamed Mwameja walioapa kutompa mkono aliyekuwa mwenyekiti wa chama cha soka nchini FAT Muhidin Ndolanga baada ya bifu lao kuanzia kwenye timu ya Taifa ya Tanzania enzi hizo wakicheza Simba.

Huko England Wayne Bridge aligoma kumpa mkono nahodha wa Chelsea John Terry,mshambuliaji wa Liverpool Luis Suarez naye amewahi kugoma kumpa mkono beki wa Manchester United Patrice Evra,Kaseja naye kaamua kutompa mkono Ivo Mapunda Tanzania wote wakicheza nafasi za golini.

Yapo matukio ya wachezaji wengi kutopeana mkono na wengine ambayo hutokea hata kwenye mechi za ligi kuu Tanzania lakini hayo ni baadhi ya matukio ya kukukumbusha.

Arsenal vs Chelsea

Picha mechi ya Arsenal dhidi ya Chelsea iliyomalizika kwa matokeo ya 0-0 huko Emirates stadium








Mtawala aachia ukatibu Simba,atambulishwa TFF leo

Aliyekuwa katibu mkuu wa Wekundu wa Msimbazi Simba Evodius Mtawala ameachana na klabu hiyo baada ya kupata kazi mpya ya ukurugenzi wa Sheria na utawala Shirikisho la soka nchini TFF.

Mtawala tayari amewataarifu rasmi Simba kuhusiana na kazi hiyo mpya aliyoipata TFF na viongozi wote wameridhia kuondoka kwenda kusaka changamoto mpya.

Akizungumza na blog ya Supermariotz Mtawala amesema ni kweli ameacha kazi rasmi Simba na amewasilisha barua akiwa tayari pia amezungumza na viongozi wote wa Simba kuhusu maamuzi yake.

"Ni kweli nimeacha kazi Simba nimepata nafasi ya kuwa Mkurugenzi wa Sheria na Utawala wa TFF kazi ambayo naiona ina changamoto mpya na naamini nitaiweza kwa kufuata sheria na kanuni" alisema.

Rais wa TFF Jamal Malinzi anamtambulisha rasmi leo mbele ya waandishi wa habari baada ya mazungumzo yote na Mtawala kukamilika na kukubali kazi hiyo ambayo ni nafasi mpya ya uongozi ndani ya TFF.

Hivi karibuni Mtawala aliapishwa rasmi kuwa mwanasheria.

*www.supermariotz.blogspot.com inampa hongera Mtawala na kumtakia kila la kheri katika kazi yake mpya,tunaamini ni kijana mdogo mwenye uelewa na uwezo mkubwa wa kazi na nafasi hiyo ataimudu.

Monday, December 23, 2013

Adebayor amzodoa Villas Boas


Mshambuliaji Emmanuel Adebayor ameendelea kumzodoa kwa kumuweka benchi aliyekuwa kocha wa Tottenham Andre Villas Boas aliyetimuliwa kazi.

Adebayor ameanza kupata nafasi ya kucheza katika kikosi hicho tokea kuondoka kwa AVB na katika mechi zote alicheza baada ya kuondoka kocha huyo ametumbukia wavuni.
Katika mchezo wa jana wa ligi kuu Adebayor ametumbukia wavuni mara mbili na kuisaidia Tottenham kuichapa Southampton wakiwa chini ya kocha Tim Sherwood.

BREAKING NEWS : Yanga wamtimua kocha Brandts

Timu ya Yanga imetangaza rasmi kumtimua kocha wake mkuu raia wa Uholanzi Ernie Brandts ikiwa ni siku chache baada ya kula kibano cha mabao 3-1 kutoka kwa mahasimu wao Wekundu wa Msimbazi Simba kwenye mchezo wa hisani wa Nani Mtani Jembe.

Akitangaza maamuzi magumu yaliyofikiwa na kamati ya utendaji Mwenyekiti wa kamati ya mashindano ya klabu hiyo ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya usajili Abdallah Binkleb amesema wamefikia uamuzi wa kumtimua kazi Brandts kwakuwa tayari uwezo wake ulifikia mwisho.

Yanga walimuongeza mkataba kocha huyo hivi karibuni na wameamua kuuvunja kwa kutoridhishwa na kiwango kinachooneshwa na timu hiyo licha ya kufanya usajili wa kuboresha kikosi.

Brandts anaondoka kwenye klabu hiyo huku akiwa amewapa ubingwa wa ligi kuu msimu uliopita na akiiacha timu hiyo ikiongoza ligi mpaka mzunguko wa kwanza unamalizika.

Kocha msaidizi Fred Felix Minziro na kocha wa makipa Razak Siwa wao wanaendelea kubakia katika timu hiyo.

Itakumbukwa Brandts alitua Yanga akitokea APR ya Rwanda msimu mmoja nyuma.

Friday, December 20, 2013

Ribery awalamba kisogo Algeria,kisa mapenzi ya mke wake


NYOTA wa Ufaransa anayecheza Bayern Munich Frank Ribery amedai kuwa timu ya Taifa ya Algeria itasonga mbele katika hatua ya makundi kombe la dunia licha ya kuwepo kwenye kundi H ambalo ni gumu.

Ribery mwenye miaka 30 amemuoa mwanamke wa kutoka Algeria Wahiba Belhami,na amekuwa akionesha kuizunga mkono timu za taifa za nchi hiyo za wadogo na ile ya wakubwa.

Anasema kama inavyofahamika mke wake ni raia wa Algeria na siku zote anamuunga mkono na ana furaha na watu wa nchi hiyo kwa timu yao kufuzu.

Algeria imepangwa na Russia, Belgium na South Korea katika kundi H,kundi linaloonekana kuwa gumu lakini Ribery anaamini timu hiyo iotafanya vizuri.

Anasema Algeria haitakiwi kujipa presha na kikubwa kucheza mchezo wao wa siku zote kwakuwa wanawachezaji ambao pia wanaviwangio vinavyostahili.

Algeria watafungua pazia kwa kucheza dhidi ya Belgium June 17 mwakani huko Estadio Mineirao mjini Belo Horizonte.

Thursday, December 19, 2013

Mputu agomea CHAN,atoa masharti kwa FA


Mkali wa kutumbukia wavuni wa DR Congo Tresor Mabe Mputu ametishia kujiondoa kwenye kikosi cha nchi hiyo kitakachocheza kwenye fainali za mataifa bingwa barani Africa CHAN nchini Africa Kusini.

Mshambuliaji huyo wa TP Mazembe mwenye miaka 28 amesema hatashiriki katika michuano hiyo kama mamlaka husika ya soka haitarekebisha hali za wachezaji wa ndani.

Amesema hatakwenda kwenye fainali hizo kwakuwa FA haiwaheshimu wachezaji wa ndani na kuna kutokuwepo kwa mipango kwa timu hiyo inayokwenda CHAN.

Anasema kama madai hayo yatawekwa sawa kabla ya fainali hizo atakubali kuiwakilisha nchi yake.



Wednesday, December 18, 2013

Rage atuma Polisi kuzuia mkutano wa viongozi,Polisi wawaweka chini ya ulinzi wachemsha waondoka kimya kimya


Mwenyekiti wa Simba Ismail Aden Rage ametuma Polisi kuzuia mkutano wa viongozi wa matawi uliokuwa unafanyika kwenye makao makuu ya klabu hiyo jioni hii.

Mkutano huo ulioitishwa na Kaimu makamu mwenyekiti Swedy Nkwabi uliwakutanisha viongozi wa matawi yote ya Simba kujadili mchezo wao wa Jumamosi wa Mtani Jembe dhidi ya mahasimu wao Yanga utakaopigwa uwanja wa Taifa.

Wakati mkutano huo ukiendelea viongozi hao wakajikuta wakiwekwa chini ya ulinzi wa Polisi walioongozwa na OCD wa kituo cha Polisi Msimbazi ambapo waliweka bayana kuwa wametumwa na mwenyekiti wa klabu hiyo Rage kuzuia mkutano huo kwakuwa haukuwa wa amani.

Viongozi hao wa matawi wakawaeleza ukweli Polisi wakisema ni mkutano wa amani na ndio maana hata wao walipofika hawakukuta vurugu zozote na ndipo Polisi hao walipolazimika kumpigia simu mwenyekiti huo ambaye alipoelezwa hakuna uvunjifu wa amani akageuza kibao na kusema hataki tawi la Mpira Pesa liwepo kwenye mkutano huo jambo ambalo lilikosa mashiko na Polisin wakaondoka kimya kimya na mkutano kuendelea.

Katika mkutano huo pia viongozi wa matawi wamemruka mwenyekiti wao Rage wakisema hawamuungi mkono kwa kauli yake ya kutaka kuitisha uchaguzi mwezi ujao ili viongozi wote waondoke madarakani.

Mourinho awabwatukia washambuliaji wake,amuangushia zigo Torres


Boss wa Chelsea Jose Mourinho amepoteza imani kwa washambuliaji wa timu hiyo ambao wamepoteza makali ya kutumbukia wavuni.

Mourinho anasema kwasasa kwenye timu yake hana muuaji anayeweza kufikisha mabao 25 baada ya kupoteza uwezo wao wa kutumbukia wavuni.

Mourinho hakusita kumwangushia zigo Fernando Torres akisema si Yule ambaye anafahamika akiwapa shida mabeki wa timu pinzani uwezo ambao kwasasa umepotea.

Wafungaji wa Chelsea mpaka sasa,michezo waliyocheza na mabao yao
  • Fernando Torres (17 games, 6 goals this season)
  • Demba Ba (13, three)
  • Samuel Eto'o (15, 4)
  • Eden Hazard (21, 8)
  • Juan Mata (15, one)
  • Oscar (21, six)
  • Andre Schurrle (18, three)
  • Kevin De Bruyne (eight, none)
  • Willian (14, one)

Suarez kukoga fedha Liverpool


Klabu ya Liverpool imeanza mazungumzo na wakala wa Luis Suarez kuhusu mkataba mpya ambao utamfanya mshambuliaji huyo wa Uruguay kuwa mchezajji mwenye mshahara mkubwa kupita wote katika historia ya klabu hiyo.

Mkurugenzi mkuu Ian Ayre alirejea Liverpool kutoka Hispania Jumanne baada ya kufanya mazungumzo na wakala wa Suarez, Pere Guardiola.

Wamiliki wa Liverpool wameidhinisha mkataba huo lakini haijulikani kama Suarez,mwenye umri wa miaka 26, atakubali kuendelea zaidi ya mwaka 2016, wakati mkataba wake utakapomalizika.

Huenda ikahitajika mkataba wa karibu pauni 200,000 kwa wiki ikiwa mara mbili ya pato lake la sasa ili kumshawishi kusaini mkataba mpya.

Hata hivyo uhusiano wake na maafisa wakuu wa Anfield umeimarika kwa kiwango kikubwa tangu alipojaribu kulazimisha auzwe Arsenal mwanzoni mwa msimu huu.

Arsenal ilijaribu mara mbili kumnunua Suarez bila mafanikio yoyote,Lakini pia kumekuwa na fununu kwamba Real Madrid ya Hispania nao pia wanapiga hesabu za kumsajili.

Manchester United kucheza bila mashabiki Champions league



Olympiakos watacheza mchezo wao dhidi ya Manchester United ligi ya mabingwa barani Ulaya bila ya mashabiki.

Uefa imeamuru hilo kufuatia mashabiki wa kikosi hicho kuonesha vitendo vya kibaguzi,na kurusha fataki wakati wa mchezo wao waliocheza dhidi ya Anderlecht December 10.

Klabu hiyo pia imepigwa faini ya Euro elfu 30.

Manchester United watacheza na mabingwa hao wa Ugiriki February 25.

Nayo Zenit St Petersburg nao watacheza mchezo wake wa nyumbani bila ya mashabiki dhidi ya Borussia Dortmund.

Wamepewa adhabu hiyo kufuatia vurugu za mashabiki kwenye mchezo ambao waliichapa mabao 4-1 Austria Vienna.

Tuesday, December 17, 2013

Vitali Klitschko agomea kutetea taji lake la dunia,akili yake aikita kwenye siasa,aota kuwa Rais 2015

Bingwa wa dunia wa WBC Vitali Klitschko ameweka pembeni masumbwi na uwezekano wa kutetea taji lake kwasasa akiwa amejikita kwenye siasa.

Bondia huyo mwenye miaka 42 ambaye ni kiongozi wa upinzani nchini Ukraine amesema kwasasa hafikirii masumbwi kwakuwa anahisi watu wa nchini mwake wanamuhitaji zaidi.

Watu waliandamana kwa wiki nzima nchini humo katika mji wa Kiev kupinga maamuzi ya Rais wao Viktor Yanukovych kutosaini mpango wa ushirikiano wa Ulaya huku jina la Klitschko likitajwa zaidi na ana mipango ya kuwania nafasi ya Rais kwenye uchaguzi wa 2015.


El Hadary aipiga chini ofa ya Tp Mazembe,asaini Wadi Degla

Golikipa mkongwe wa Misri Essam El Hadary amesaini kuichezea Wadi Degla kwa mkataba wa miezi sita kuanzia mwezi ujao.

El Hadary amemaliza mkataba wake wa kuichezea Al Merrikh ya Sudan mwezi uliopita.

Kipa huyo mkongwe amesema amesaini mkataba huo wa miezi sita ambao utafuatiwa na kusaini mkataba mwingine baada ya kumalizika miezi sita kama pande zote zitakubaliana.

Amesema alifanya mazungumzo na timu hiyo kuanzia mwezi uliopita na wamekubali kila kitu alichohitaji.

El Hadary anaongeza kuwa kumekuwa na ofa nyingi lakini ameichagua Degla kwasababu walihitaji sana huduma yake na amewaahidi kuwafanyia makubwa.

Inaelezwa kuwa TP Mazembe ya Congo DRC ilikuwa pia ikihitaji huduma ya kipa huyo lakini ameipiga chini ofa hiyo na kurejea kwenye ligi ya nyumbani Misri.

El Hadary amewahi kuzichezea timu za Al Ahly , Zamalek na Al Ismaily zote za Misri.

Monday, December 16, 2013

Babi apata timu Malaysia,asaini mkataba wa mwaka mmoja

Kiungo Abdi Kassim Babi amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuichezea UITM FC ya Malaysia.

Babi amewashukuru viongozi wa KMKM ya Zanzibar ambayo alikuwa anaichezea kabla ya kusaini mkataba huo UITM FC.

Amewahi kucheza Yanga,Mtibwa,Azam FC,KMKM ya Zanzibar na mara kadhaa alikuwa akiitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania Taifa Starz lakini pia ni mchezaji wa timu ya taifa ya Zanzibar Zanzibar Heroes.

Kipigo cha Liverpool,Spurs yamtimua AVB

Tottenham wamemtimua kazi Andre Villas-Boas baada ya kipigo cha mabao 5-0 kutoka kwa Liverpool.
Kipigo hicho kimeifanya timu hiyo kuwa na msimu mbaya zaidi kwa kipindi cha miaka 16 na kuiacha Spurs ikikaa kwenye nafasi ya saba ikiwa ni pointi nane nyuma ya vinara Arsenal.

Villas-Boas, 36,alipewa mikoba Tottenham July 2012.

Itakumbukwa Villas-Boas alitimuliwa kazi Chelsea March 2012 baada ya kuitumikia kwa miezi nane tu na kupewa mikoba kwenye kikosi hicho na amekuwa kwenye presha kwenye siku za karibuni.

Tottenham pia kwenye msimu huu ilikula kisago cha mabao 6-0 kutoka kwa Manchester City November 24,licha ya kutoka sare na Manchester United na kushinda dhidi ya Fulham na Sunderland, kipigo kutoka kwa Liverpool kinathibitisha mwisho wa utawala wa Spurs.

Okwi uso kwa uso na Simba Mtani jembe

SIKU moja baada ya kumnasa mshambuliaji wa zamani wa Simba Emmanuel Okwi,Yanga wameweka wazi nia yao ya kuanza kumtumia mshambuliaji huyo kwenye mchezo utakaowakutanisha na mahasimu wao hao wikiendi inayokuja.

Yanga ambao wamemsainisha Okwi mkataba wa miaka miwili na nusu wamesema baada ya kukamilisha mambo mshambuliaji huyo atatua nchini Jumatano tayari kuanza majukumu yake mapya.

Okwi mwenye miaka 21 aliuzwa na Simba kwenda Etoile du Sahel ya Tunisia lakini hivi karibuni mchezaji huyo akaidhinishwa na FIFA kuichezea SC Villa ya Uganda kufuatia kuwepo mgogoro kati ya mchezaji huyo na timu yake ya Etoile ambao walishindwa kumlipa mshahara wake huku pia wakiwa wameshindwa kulipa fedha ya uhamisho dola 300,000.

Usajili wake tayari umeanza kuibua maneno maneno upande wa pili kwa mahasimu wao Simba ambao wameanza kushikana uchawi wenyewe kwa wenyewe kuhusika katika mpango huo wa kuuzwa kwa Okwi.

Azam FC yafukuza mwizi kimya kimya

Timu ya Azam FC ni kama in afukuza mwizi kimya kimya wakiwa tayari wameanza kujifua kwa mzunguko wa pili wa ligi kuu soka Tanzania bara.

Azam wanaendelea kujifua chini ya makocha Kally Ongala na Ibrahim Shikanda wakifuata programme iliyoachwa na kocha wao Joseph Omog aliyesaini mkataba hivi karibuni wa kuitumikia timu hiyo akichukua mikoba ya Sterwat John Hall.

Mzunguko wa kwanza wamemaliza wakiwa katika nafasi ya pili nyuma ya vinara Yanga Africa.
 
Kipre na Aggrey

Picha kwa hisani ya Azam FC