Monday, December 16, 2013

Babi apata timu Malaysia,asaini mkataba wa mwaka mmoja

Kiungo Abdi Kassim Babi amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuichezea UITM FC ya Malaysia.

Babi amewashukuru viongozi wa KMKM ya Zanzibar ambayo alikuwa anaichezea kabla ya kusaini mkataba huo UITM FC.

Amewahi kucheza Yanga,Mtibwa,Azam FC,KMKM ya Zanzibar na mara kadhaa alikuwa akiitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania Taifa Starz lakini pia ni mchezaji wa timu ya taifa ya Zanzibar Zanzibar Heroes.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.