Wednesday, December 18, 2013

Suarez kukoga fedha Liverpool


Klabu ya Liverpool imeanza mazungumzo na wakala wa Luis Suarez kuhusu mkataba mpya ambao utamfanya mshambuliaji huyo wa Uruguay kuwa mchezajji mwenye mshahara mkubwa kupita wote katika historia ya klabu hiyo.

Mkurugenzi mkuu Ian Ayre alirejea Liverpool kutoka Hispania Jumanne baada ya kufanya mazungumzo na wakala wa Suarez, Pere Guardiola.

Wamiliki wa Liverpool wameidhinisha mkataba huo lakini haijulikani kama Suarez,mwenye umri wa miaka 26, atakubali kuendelea zaidi ya mwaka 2016, wakati mkataba wake utakapomalizika.

Huenda ikahitajika mkataba wa karibu pauni 200,000 kwa wiki ikiwa mara mbili ya pato lake la sasa ili kumshawishi kusaini mkataba mpya.

Hata hivyo uhusiano wake na maafisa wakuu wa Anfield umeimarika kwa kiwango kikubwa tangu alipojaribu kulazimisha auzwe Arsenal mwanzoni mwa msimu huu.

Arsenal ilijaribu mara mbili kumnunua Suarez bila mafanikio yoyote,Lakini pia kumekuwa na fununu kwamba Real Madrid ya Hispania nao pia wanapiga hesabu za kumsajili.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.