Wednesday, December 18, 2013

Rage atuma Polisi kuzuia mkutano wa viongozi,Polisi wawaweka chini ya ulinzi wachemsha waondoka kimya kimya


Mwenyekiti wa Simba Ismail Aden Rage ametuma Polisi kuzuia mkutano wa viongozi wa matawi uliokuwa unafanyika kwenye makao makuu ya klabu hiyo jioni hii.

Mkutano huo ulioitishwa na Kaimu makamu mwenyekiti Swedy Nkwabi uliwakutanisha viongozi wa matawi yote ya Simba kujadili mchezo wao wa Jumamosi wa Mtani Jembe dhidi ya mahasimu wao Yanga utakaopigwa uwanja wa Taifa.

Wakati mkutano huo ukiendelea viongozi hao wakajikuta wakiwekwa chini ya ulinzi wa Polisi walioongozwa na OCD wa kituo cha Polisi Msimbazi ambapo waliweka bayana kuwa wametumwa na mwenyekiti wa klabu hiyo Rage kuzuia mkutano huo kwakuwa haukuwa wa amani.

Viongozi hao wa matawi wakawaeleza ukweli Polisi wakisema ni mkutano wa amani na ndio maana hata wao walipofika hawakukuta vurugu zozote na ndipo Polisi hao walipolazimika kumpigia simu mwenyekiti huo ambaye alipoelezwa hakuna uvunjifu wa amani akageuza kibao na kusema hataki tawi la Mpira Pesa liwepo kwenye mkutano huo jambo ambalo lilikosa mashiko na Polisin wakaondoka kimya kimya na mkutano kuendelea.

Katika mkutano huo pia viongozi wa matawi wamemruka mwenyekiti wao Rage wakisema hawamuungi mkono kwa kauli yake ya kutaka kuitisha uchaguzi mwezi ujao ili viongozi wote waondoke madarakani.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.