SIKU moja baada ya kumnasa mshambuliaji wa zamani wa Simba Emmanuel Okwi,Yanga wameweka wazi nia yao ya kuanza kumtumia mshambuliaji huyo kwenye mchezo utakaowakutanisha na mahasimu wao hao wikiendi inayokuja.
Yanga ambao wamemsainisha Okwi mkataba wa miaka miwili na nusu wamesema baada ya kukamilisha mambo mshambuliaji huyo atatua nchini Jumatano tayari kuanza majukumu yake mapya.
Okwi mwenye miaka 21 aliuzwa na Simba kwenda Etoile du Sahel ya Tunisia lakini hivi karibuni mchezaji huyo akaidhinishwa na FIFA kuichezea SC Villa ya Uganda kufuatia kuwepo mgogoro kati ya mchezaji huyo na timu yake ya Etoile ambao walishindwa kumlipa mshahara wake huku pia wakiwa wameshindwa kulipa fedha ya uhamisho dola 300,000.
Usajili wake tayari umeanza kuibua maneno maneno upande wa pili kwa mahasimu wao Simba ambao wameanza kushikana uchawi wenyewe kwa wenyewe kuhusika katika mpango huo wa kuuzwa kwa Okwi.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.