Aliyekuwa katibu mkuu wa Wekundu wa Msimbazi Simba Evodius Mtawala
ameachana na klabu hiyo baada ya kupata kazi mpya ya ukurugenzi wa
Sheria na utawala Shirikisho la soka nchini TFF.
Mtawala
tayari amewataarifu rasmi Simba kuhusiana na kazi hiyo mpya aliyoipata
TFF na viongozi wote wameridhia kuondoka kwenda kusaka changamoto mpya.
Akizungumza
na blog ya Supermariotz Mtawala amesema ni kweli ameacha kazi rasmi
Simba na amewasilisha barua akiwa tayari pia amezungumza na viongozi
wote wa Simba kuhusu maamuzi yake.
"Ni kweli nimeacha kazi
Simba nimepata nafasi ya kuwa Mkurugenzi wa Sheria na Utawala wa TFF
kazi ambayo naiona ina changamoto mpya na naamini nitaiweza kwa kufuata
sheria na kanuni" alisema.
Rais wa TFF Jamal Malinzi
anamtambulisha rasmi leo mbele ya waandishi wa habari baada ya
mazungumzo yote na Mtawala kukamilika na kukubali kazi hiyo ambayo ni
nafasi mpya ya uongozi ndani ya TFF.
Hivi karibuni Mtawala aliapishwa rasmi kuwa mwanasheria.
*www.supermariotz.blogspot.com
inampa hongera Mtawala na kumtakia kila la kheri katika kazi yake
mpya,tunaamini ni kijana mdogo mwenye uelewa na uwezo mkubwa wa kazi na
nafasi hiyo ataimudu.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.