Bingwa wa dunia wa WBC Vitali Klitschko ameweka pembeni masumbwi na uwezekano wa kutetea taji lake kwasasa akiwa amejikita kwenye siasa.
Bondia huyo mwenye miaka 42 ambaye ni kiongozi wa upinzani nchini Ukraine amesema kwasasa hafikirii masumbwi kwakuwa anahisi watu wa nchini mwake wanamuhitaji zaidi.
Watu waliandamana kwa wiki nzima nchini humo katika mji wa Kiev kupinga maamuzi ya Rais wao Viktor Yanukovych kutosaini mpango wa ushirikiano wa Ulaya huku jina la Klitschko likitajwa zaidi na ana mipango ya kuwania nafasi ya Rais kwenye uchaguzi wa 2015.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.