Monday, December 16, 2013

Kipigo cha Liverpool,Spurs yamtimua AVB

Tottenham wamemtimua kazi Andre Villas-Boas baada ya kipigo cha mabao 5-0 kutoka kwa Liverpool.
Kipigo hicho kimeifanya timu hiyo kuwa na msimu mbaya zaidi kwa kipindi cha miaka 16 na kuiacha Spurs ikikaa kwenye nafasi ya saba ikiwa ni pointi nane nyuma ya vinara Arsenal.

Villas-Boas, 36,alipewa mikoba Tottenham July 2012.

Itakumbukwa Villas-Boas alitimuliwa kazi Chelsea March 2012 baada ya kuitumikia kwa miezi nane tu na kupewa mikoba kwenye kikosi hicho na amekuwa kwenye presha kwenye siku za karibuni.

Tottenham pia kwenye msimu huu ilikula kisago cha mabao 6-0 kutoka kwa Manchester City November 24,licha ya kutoka sare na Manchester United na kushinda dhidi ya Fulham na Sunderland, kipigo kutoka kwa Liverpool kinathibitisha mwisho wa utawala wa Spurs.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.