Thursday, December 19, 2013

Mputu agomea CHAN,atoa masharti kwa FA


Mkali wa kutumbukia wavuni wa DR Congo Tresor Mabe Mputu ametishia kujiondoa kwenye kikosi cha nchi hiyo kitakachocheza kwenye fainali za mataifa bingwa barani Africa CHAN nchini Africa Kusini.

Mshambuliaji huyo wa TP Mazembe mwenye miaka 28 amesema hatashiriki katika michuano hiyo kama mamlaka husika ya soka haitarekebisha hali za wachezaji wa ndani.

Amesema hatakwenda kwenye fainali hizo kwakuwa FA haiwaheshimu wachezaji wa ndani na kuna kutokuwepo kwa mipango kwa timu hiyo inayokwenda CHAN.

Anasema kama madai hayo yatawekwa sawa kabla ya fainali hizo atakubali kuiwakilisha nchi yake.



No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.