Tuesday, December 24, 2013
EXCLUSIVE : Sina bifu na Ivo-Kaseja
GOLIKIPA wa Yanga Africa aliyewahi kucheza Simba Juma Kaseja amefunguka kuhusu suala la kutompa mkono golikipa wa Simba aliyewahi kucheza Yanga Ivo Mapunda.
Kaseja amesema tofauti na watu wanavyofikiri lakini yeye kwa upande wake hana bifu lolote wala chuki na Ivo na kwake ilikuwa kitu cha kawaida.
"Unajua kaka watu wanaongea sana lakini mimi sina bifu lolote na Ivo,hivyo ni vitu vya kawaida tu na maamuzi ya mtu" alisema Kaseja.
Amesema kuwa hakuwa na sababu yoyote ya kutompa mkono Ivo zaidi ya kuamua kufanya hivyo kwasababu yale ni maamuzi yake binafsi na si sababu ya bifu au chuki baina yao.
Kaseja si mchezaji wa kwanza kutopeana mikono na mchezaji mwenzake au kiongozi wakati wa kusalimiana kabla ya kuanza kwa mchezo,imewahi kutokea kwa Steven Mapunda na Mohamed Mwameja walioapa kutompa mkono aliyekuwa mwenyekiti wa chama cha soka nchini FAT Muhidin Ndolanga baada ya bifu lao kuanzia kwenye timu ya Taifa ya Tanzania enzi hizo wakicheza Simba.
Huko England Wayne Bridge aligoma kumpa mkono nahodha wa Chelsea John Terry,mshambuliaji wa Liverpool Luis Suarez naye amewahi kugoma kumpa mkono beki wa Manchester United Patrice Evra,Kaseja naye kaamua kutompa mkono Ivo Mapunda Tanzania wote wakicheza nafasi za golini.
Yapo matukio ya wachezaji wengi kutopeana mkono na wengine ambayo hutokea hata kwenye mechi za ligi kuu Tanzania lakini hayo ni baadhi ya matukio ya kukukumbusha.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.