Wednesday, December 18, 2013

Manchester United kucheza bila mashabiki Champions league



Olympiakos watacheza mchezo wao dhidi ya Manchester United ligi ya mabingwa barani Ulaya bila ya mashabiki.

Uefa imeamuru hilo kufuatia mashabiki wa kikosi hicho kuonesha vitendo vya kibaguzi,na kurusha fataki wakati wa mchezo wao waliocheza dhidi ya Anderlecht December 10.

Klabu hiyo pia imepigwa faini ya Euro elfu 30.

Manchester United watacheza na mabingwa hao wa Ugiriki February 25.

Nayo Zenit St Petersburg nao watacheza mchezo wake wa nyumbani bila ya mashabiki dhidi ya Borussia Dortmund.

Wamepewa adhabu hiyo kufuatia vurugu za mashabiki kwenye mchezo ambao waliichapa mabao 4-1 Austria Vienna.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.