Thursday, October 31, 2013

Mabomu ya machozi yarindima uwanja wa Taifa,Simba ikishikwa na Kagera,mashabiki wavunja viti


Kuvunjwa kwa viti na kupigwa kwa mabomu ya machozi ni moja ya matukio yaliyotokea kwenye mchezo wa ligi kuu soka Tanzania bara kati ya wekundu wa Msimbazi Simba dhidi ya Kagera Sugar wana Nkurukumbi uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa Dar Es Salaam uliomalizika kwa sare ya kufungana bao 1-1.

Polisi walilazimika kupiga mabomu ya machozi baada ya mashabiki wa Simba kuanzisha vurugu na kuvunja viti vya uwanja huo hali iliyolazimu kuanza kupigwa kwa mabomu ya machozi ili kuwatawanya mashabiki hao.

Mpaka viti vinavunjwa na mabomu yanaanza kupigwa Simba na Kagera walikuwa wamefungana bao 1-1.

Bao la Simba limefungwa na Amis Tambwe wakati lile la Kagera lilipachikwa wavuni na Salum Kanoni Kupela kwa mkwaju wa penati baada ya kuangushwa ndani ya kisanduku kwa mshambuliaji Adam Kingwande.

Simba sasa wanafikisha pointi 21 wakiendelea kukaa nyuma ya Azam FC,Mbeya City wenye pointi 23 na Yanga wenye pointi 22 huku Simba akicheza mchezo mmoja zaidi.

Simba mikononi mwa Kagera Sugar,..kurushwa live Channel ten,TBC2

Wekundu wa Msimbazi Simba leo wanashuka dimbani kusaka pointi tatu muhimu za kutuliza mzuka huko Msimbazi baada ya kupata kipigo cha mabao 2-1 katika mchezo uliopita dhidi ya Azam FC.

Simba wanashuka kuwakabili Kagera Sugar wana Nkurukumbi kwenye uwanja wa Taifa katika mchezo muhimu wa ligi kuu ya Tanzania bara.

Wekundu hao wanashuka dimbani huku wakiwa wameshushwa kwenye msimamo wa ligi mpaka nafasi ya nne kufuatia Azam,Mbeya City na Yanga kushinda katika michezo yao iliyopita.

Azam wanaongoza wakiwa na pointi 23 sawa na Mbeya City,huku Yanga akikaa nafasi ya tatu akiwa na pointi 22 na Simba wapo nafasi ya nne wakiwa na pointi 20.

Mchezo huo utarushwa moja kwa moja na Azam Tv kupitia TBC2 na Channel ten.

Bale,Ronaldo,Benzema wang'ara Real ikimpiga mtu 7

Mshambuliaji raia wa Wales Gareth Bale ametupia mabao mawili huku akitoa pasi mbili za mabao Cristiano Ronaldo akitumbukia mara atatu na Karim Benzema akitupia mawili wakati Real Madrid ilipoichapa Sevilla 7-3 kwenye mchezo wa ligi kuu ya Hispania La liga.

Ivan Rakitic amefunga mabao mawili na Carlos Bacca akafunga moja kwa upande wa Sevilla,ambao walishuhudia MCameroon wao Stephane Mbia akilimwa kadi nyekundu.

Real Madrid wana pointi 6 nyuma ya vinara Barcelona.

Matokeo mengine ya La liga


Wed 30 Oct 2013 - Spanish La Liga
  • Real Valladolid 2 - 2 Real Sociedad FT
  • Valencia CF 1 - 2 Almería FT
  • Osasuna 3 - 1 Rayo Vallecano FT
Tue 29 Oct 2013 - Spanish La Liga

Wednesday, October 30, 2013

Real Madrid yamtoa sadaka Benzema impate Suarez

REAL MADRID wanajipanga kwa usajili wa dirisha dogo mwezi January kutumbukia kumnasa Luis Suarez wa Liverpool kwa dau la paundi milioni 20 pamoja na mshambuliaji Karim Benzema.

Suarez bado inaelezwa anataka kuondoka Anfield,licha ya mwanzo mzuri wa msimu kwa Liverpool.

Arsenal nao wanajipanga kwa dau lingine baada ya kutolewa nje kwenye usajili uliopita wa majira ya joto.

Lakini Suarez inaonekana anapenda zaidi kwenda Real Madrid inayofundishwa na Carlo Ancelotti na wakali hao wa Hispania wana matumaini ya kuwashawishi Liverpool kwa kuwapa fedha na mchezaji mwenye jina kubwa Benzema.

Madrid wanaona thamani ya Benzema ni paundi milioni 20 inayofanya mpango huo kuwa na jumla ya paundi milioni 40.
 

Benzema tayari anaonekana kupoteza thamani yake ndani ya Real Madrid na tayari ameambiwa anaweza kuondoka na kusaka timu nyingine.

Madrid wametumia kiasi cha paundi milioni 150 kwenye usajili wake ikiwemo paundi milioni 86 walizozitoa kumnunua Gareth Bale aliyeweka rekodi ya dunia kwakuwa mchezaji ghali zaidi.


Fabio Coentrao, Sami Khedira na Angel Di Maria ni miongoni mwa wale wanaotajwa kuwa sehemu ya kuuwezesha mpango wa kumnasa Suarez.
 
 

Balotelli kumfuata Mourinho Chelsea

Mshambuliaji wa zamani wa MANCHESTER CITY Mtaliano Mario Balotelli anaweza akafanya uhamisho wa kushtua kuhamia Chelsea kwa mujibu wa wakala wake.

Balotelli,ambaye kwasasa anacheza AC Milan alikuwa pamoja na Jose Mourinho kwenye timu ya Inter Milan mwaka 2009.

Wakala wa Balotelli Mino Raiola amesema upo uwezekano mkubwa wa mshambuliaji huyo kuungana tena na Mourinho kwakuwa wawili hao hawakuachana kwa matatizo.

Anasema hakukuwa na matukio mazuri baina ya wawili hao lakini pia waliachana kwa makubaliano mazuri,kuna mawasiliano wanafanya na kuna heshima kati yao.

Wakala huyo anasema anafahamu makamu wa Rais wa AC Milan Adriano Galliani hatakubali lakini Balotelli ni mchezaji mkubwa.

Balotelli amefunga mabao 6 kwa klabu na timu yake ya Taifa kwa msimu huu.

CAF yampa tano Malinzi

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), Issa Hayatou amempongeza Jamal Malinzi kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) katika uchaguzi uliofanyika Oktoba 27 mwaka huu.

Katika salamu zake kwa niaba ya Kamati ya Utendaji ya CAF na familia ya mpira wa miguu Afrika, Rais Hayatou amesema uchaguzi huo unampa Rais Malinzi fursa ya kuupeleka mbele mpira wa miguu nchini Tanzania.

Amesema CAF ina imani uwezo wake katika uongozi, uzoefu na ujuzi katika mpira wa miguu havitausaidia mpira wa miguu Tanzania pekee bali Afrika kwa ujumla, na kuongeza kuwa ataendeleza ushirikiano uliopo ili kuwanufaisha zaidi vijana wa bara hili.

Rais Hayatou amemtakia Rais Malinzi kila la kheri katika kipindi chake cha uongozi na kumhakikishia kuwa CAF iko pamoja naye katika kusukuma mbele gurudumu la kuendeleza mpira wa miguu.


Tuesday, October 29, 2013

Baada ya ushindi Mbeya City wavunja vioo vya magari ya Tz Prisons

Baada ya kumalizika kwa mchezo wa ligi kuu ya Tanzania bara kwenye uwanja wa Sokoine Mbeya mchezo wa mahasimu Mbeya City dhidi ya Tanzania Prisons uliomalizika kwa Mbeya City kushinda mabao 2-0,mashabiki wanaosadikika kuwa wa Mbeya City wamevunja vioo vya magari ya Prisons.

Tazama picha :
 
 
 
 
 
Picha kwa hisani ya blog ya Mbeya Yetu.

VPL : Mbeya City mwendo mdundo,Yanga yafanya kweli,Simba mmh


Ligi kuu ya soka Tanzania bara imeendelea tena leo kwa michezo mitatu kuchezwa katika viwanja tofauti ambapo katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam, mabingwa watetezi Yanga Africa waliwaalika maafande wa Mgambo kutoka Handeni huko Tanga.

Huko Sokoine mjini Mbeya kulikuwa na mchezo wa mahasimu wa mkoa huo Mbeya City dhidi ya Tanzania Prisons,wakati huko Taboa kwenye uwanja wa Ally Hassan Mwinyi Rhino Rangers wamecheza na JKT Ruvu.

Uwanja wa Taifa Yanga Africa wamefanikiwa kukalia nafasi ya tatu juu ya mahasimu wao Wekundu wa msimbazi Simba kufuatia kupata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Mgambo shooting.

Mabao ya Yanga walitupiwa wavuni na Mbuyu Twite,Hamis Kiiza Diego na Didier kavumbagu.

Ushindi huo umewafanya Yanga kufikisha pointi 22 ambazo ni pointi mbili zaidi ya mahasimu wao Simba wenye pointi 20 ambao jana walikubali kichapo cha mabao 2-1 kutoka wa waoka mikate wa Azam FC.

Mchezo mwingine wa ligi kuu uliounguruma leo ilikuwa huko Mbeya katika uwanja wa kumbu kumbu ya Sokoine mahasimu Mbeya City na Tanzania Prisons walioneshana kazi na matokeo tuliyoyapata kutoka Mbeya timu ya Mbeya City imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 ushindi uonawafanya kuendelea kukimbizana na Azam FC kileleni mwa ligi hiyo wote wakiwa na pointi 23 wakitofautiana mabao ya kufunga na kufungwa.

Ronaldo,Messi vita nyingine tuzo za Ballon d'Or

Shirikisho la soka duniani FIFA limewajumuisha wachezaji 6 wa klabu ya Bayern Munich kwenye orodha ya wachezaji wengine 23 watakaowania tuzo la mchezaji bora duniani mwaka huu Ballon d'Or .

Jose Mourinho amejumuishwa kwenye orodha ya kocha bora licha ya kukosa kuiwezesha klabu ya Real Madrid kushinda taji lolote kubwa msimu uliopita, matokeo ambayo aliyataja kuwa mabovu.
Mchezaji wa pekee kutoka Uingereza ambaye ameteuliwa ni mchezaji wa kimataifa wa Wales, Gareth Bale.
Mshindi wa tuzo ya kocha bora Afrika Stephen Keshi wa Nigeria hakufanikiwa kuwa kwenye orodha hiyo huku mwafrika pekee kuteuliwa kuwania taji hilo akiwa Yaya Toure mchezaji wa kiungo cha kati wa Manchester City raia wa Ivory Coast.
Kwenye orodha hiyo hamna wawakilishi kutoka Asia ama CONCACAF

Wachezaji wa kimataifa kutoka Ujerumani Manuel Neuer, Bastian Schweinsteiger , Thomas Mueller na Phillip Lahm pamoja na mfaransa Franck Ribery na mchezaji wa Uholanzi Arjen Robben ndio wachezaji wa Bayern walioteuliwa.

Wengine waliojumuishwa kwenye orodha hiyo ni wachezaji maarufu kama Lionel Messi, Andres Ineasta na Cristiano Ronaldo.
 
Aliyekuwa kocha wa Bayern Jupp Heynckes ambaye nafasi yake imechukuliwa na Pep Guardiola ameteuliwa kwenye orodha ya kocha bora baada ya kuiongoza klabu yake kushinda ligi ya ujerumani ya Bundesliga, kombe la ujerumani na ligi ya mabingwa barani Ulaya.


Fifa world men's player of the year shortlist: Gareth Bale (Real Madrid/Wales), Edinson Cavani (Paris St-Germain/Uruguay), Radamel Falcao (Monaco/Colombia), Eden Hazard (Chelsea/Belgium), Zlatan Ibrahimovic (Paris St-Germain/Sweden), Andres Iniesta (Barcelona/Spain), Philipp Lahm (Bayern Munich/Germany), Robert Lewandowski (Borussia Dortmund/Poland), Lionel Messi (Barcelona/Argentina), Thomas Muller (Bayern Munich/Germany), Manuel Neuer (Bayern Munich/Germany), Neymar (Barcelona/Brazil), Mesut Ozil (Arsenal/Germany), Andrea Pirlo (Juventus/Italy), Franck Ribery (Bayern Munich/France), Arjen Robben (Bayern Munich/Netherlands), Cristiano Ronaldo (Real Madrid/Portugal), Bastian Schweinsteiger (Bayern Munich/Germany), Luis Suarez (Liverpool/Uruguay), Thiago Silva (Paris St-Germain/Brazil), Yaya Toure (Manchester City/Ivory Coast), Robin Van Persie (Manchester United/Netherlands), Xavi (Barcelona/Spain).
Fifa coach of the year shortlist: Carlo Ancelotti (Real Madrid), Rafael Benítez (Napoli), Antonio Conte (Juventus), Vicente Del Bosque (Spain), Sir Alex Ferguson (Manchester United's former manager), Jupp Heynckes (Bayern Munich's former coach), Jurgen Klopp (Borussia Dortmund), Jose Mourinho (Chelsea), Luiz Felipe Scolari (Brazil), Arsene Wenger (Arsenal).

Formula1 : Mercedes yamegeka


Ross Brawn ataacha kuiongoza timu ya Mercedes ya kwenye mashindano ya magari ya langalanga ya Formula One, kufikia mwisho wa msimu huu.

Brawn na timu hiyo ya Mercedes wameshindwa kuafikiana kuhusu wajibu wake katika timu hiyo, kulingana na taarifa za kuaminika kutoka timu hiyo ya mashindano ya magari.
Timu ya Mercedes sasa itaongozwa na wakurugenzi wawili watakaoshirikiana pamoja, Toto Wolff na Paddy Lowe, na vile vile kutoka kwa Niki Lauda, ambaye ni mwenyekiti mkuu asiyekuwa na mamlaka rasmi ya kufanya uamuzi katika kuiendesha timu hiyo.

Mercedes, na hata Brawn, walikataa kuzungumza kuhusu kinachoendelea kati yao.
Hatua ya kuamua kuondoka kwa Brawn inaafikiwa baada ya miezi mingi ya kushauriana na wakuu wa timu ya Mercedes.

Brawn, ndiye aliyechangia umaarufu wa Mjerumani Michael Schumacher kuweza kulinyakua taji la dunia mara saba katika mashindano ya langalanga, wakati alipokuwa mkuu wa timu za Benetton na  Ferrari.
Brawn pia alihusika katika ushindi wa Jenson Button, alipoibuka bingwa wa msimu wa mwaka 2009, na alipojisajili kama mtu binafsi asiyekuwa na kampuni, kwa jina Brawn GP , kufuatia timu ya Honda kujiondoa katika mchezo huo. Hatimaye timu ya Mercedes ilimchukua mwaka 2010

CAPITAL ONE CUP : Arsenal,Chelsea hatariiiiii...Man U nao mzigoni.

Arsenal watakuwa bila ya Mikel Arteta anayetumikia adhabu na majeruhi Mathieu Flamini.

Jack Wilshere yuko fit,lakini Serge Gnabry alikuwa na tatizo la ankle ambalo anapigana nalo kuwa fit.

Boss wa Chelsea Jose Mourinho bila shaka naye atabadili kikosi katika mchezo huo wa pili ndani ya siku tatu.

Juan Mata, Kevin De Bruyne, Michael Essien, Demba Ba na Mark Schwarzer huenda leo wakapata nafasi ya kuanza kikosini.

Mechi nyingine za leo

Monday, October 28, 2013

Malinzi ndiye boss mpya TFF


Shirikisho la sloka nchini TFF hatimaye limepata viongozi wapya watakaoliongoza kwa miaka minne kufuatia uchaguzi uliofanyika kwenye ukumbi wa NSSF Water Front.

Jamal Malinzi ndiye Rais mpya wa TFF baada ya kumshinda mpinzani wake Athuman Nyamlani.

Malinzi amepata ushindi wa kura 73 akimshinda Nyamlani aliyepata kura 52.
Wallace Karia amefanikiwa kushinda nafasi ya makamu wa Rais baada ya kujikusanyia kura 67 akiwashinda Ramadhan Nassib aliyepata kura 52 na Iman Madega aliyepata kura 6.

VPL : Simba vs Azam FC hapatoshi Taifa


Ligi kuu ya Tanzania bara leo itaendelea katika raundi ya 11 ambayo ilifanyiwa marekebisho kupisha mchezo wa kutafuta tiketi ya kucheza fainali za kombe la dunia kwa wanawake kati ya timu ya taifa ya Tanzania chini ya miaka 20 dhidi ya Msumbiji.

Marekebisho hayo ya ratiba yamegusa pia raundi zote mbili zilizobaki kukamilisha mzunguko wa kwanza.

Mechi za leo

Coastal Union vs Mtibwa Sugar

Oljoro JKT vs Ashanti United

Ruvu Shooting vs Kagera Sugar

Simba vs Azam FC.

Hapo kesho Oktoba 29

Tanzania Prisons vs Mbeya City

Yanga vs Mgambo Shooting

Rhino Rangers vs JKT Ruvu

Torreeeeeeeeeeees....

Torres alipofanya yake kuwabeba Chelsea kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Manchester City ligi kuu England ngoma ikipigwa Stamford Bridge.
Bao la kwanza lililofungwa na Schurrle
 
 
 
 
Torreeeeeeeeees...
 
Mourinho akapagawa
Matokeo EPL
Sun 27 Oct 2013 - Premier League
Sat 26 Oct 2013 - Premier League

Sunday, October 27, 2013

Man U yasita kutoa dau kubwa kwa Rooney,Spurs,Arsenal watiana pembe,Mourinho kicheko

Sababu ya Manchester United kutokubaliana mkataba mpya na Wayne Rooney ni kutotaka kujitia kitanzi cha kumpa dau nono la paundi milioni 70 ili mshambuliaji huyo abaki Old Trafford.

Rooney anataka mshahara wake uongezeke kutoka ule wa sasa anaolipwa paundi 250,000 kwa wiki na anataka mkataba wa miaka mitano ili abakie.
Licha ya kiwango cha Rooney kuwa juu kwasasa baada ya kuporomoka baada ya mtifuano wake na kocha aliyeondoka Sir Alex Ferguson,bado klabu hiyo haitaki kutumia kitita kikubwa kwa mchezaji ambaye tayari ana miaka 28.

Rooney alikataliwa kuondoka kwenye usajili uliopita huku tayari Chelsea na Paris St Germain zikiwa zimemtolea macho na kocha wa sasa David Moyes akasema mshambuliaji huyo hauzwi kwa Chelsea ambao walipeleka ofa tatu na sasa inaonekana kwenye usajili wa dirisha dogo mwezi January inaweza kuibuka tena.
Upande mwingine Arsenal wako tayari kupigana na Tottenham kwa mshambuliaji wa Aston Villa Christian Benteke wakati wa usajili wa dirisha dogo mwezi January.

The Gunners wanaendelea na kampeni zake za kulisaka taji msimu huu japo inaonekana inahitaji mshambuliaji mwenye kiwango cha dunia ili kutimiza lengo lake.
 
Naye mshambuliaji wa Real Madrid aliyepoteza mvuto Karim Benzema anaweza kutua kwenye ligi ya England kwa dau la paundi milioni 42.

Madrid wanataka kurudisha sehemu ya fedha walizotoa kumnunua Gareth Bale kwa kumuuza Benzema na inaelezwa kuwa klabu za Tottenham, Arsenal na Chelsea zimepewa taarifa za uwepo wa mshambuliaji huyo.
Hata hivyo Arsenal na Spurs wanaonekana kutoa jicho zaidi kwa Benteke wakati Chelsea kocha wake Jose Mourinho amesema safu yake ya ushambuliaji anaona imeimarika zaidi na ana imani nayo.