Tuesday, October 15, 2013

Kocha wa Senegal afariki

Kocha wa zamani wa Senegal Bruno Metsu,aliyeiongoza nchi hiyo ya Africa kutinga robo fainali ya kombe la dunia 2002,amefariki akiwa na umri wa miaka 59.

Kwa mujibu wa magazeti ya La Voix du Nord,L'Equipe na France Football magazine yameripoti kuwa Metsu,ambaye aliachana na kazi ya ukocha wakati akiifundisha  klabu ya Al Wasl ya Dubai mwaka uliopita ili kupambana na kansa ya tumbo amefariki usiku wa kuamkia leo huko Dunkirk Ufaransa Kaskazini.

Metsu"The White Sorcerer",amewahi kufundisha Guinea, Qatar,na klabu kadhaa.

Jina lake lilikamata sana katika fainali za dunia 2002 Senegal ilipowachapa mabingwa watetezin wakati huo France katika mchezo wa ufunguzi na timu ikafika mpaka hatua ya robo fainali na katika mwaka huo pia Senegal ilifika fainali kwenye fainali za Africa.


No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.