Saturday, October 5, 2013
Furmula1 : Vettel amvuruga Hamilton
Sebastian Vettel amemuongoza dereva mwenzake Mark Webber wote kutoka Red Bull kushinda katika majaribio ya pili ya Korean Grand Prix.
Dereva wa Mercedes Nico Rosberg na Lewis Hamilton wamemaliza katika nafasi ya tatu na ya nne mbele ya dereva wa Ferrari Fernando Alonso na dereva wa Lotus Romain Grosjean.
Dereva wa Ferrari Felipe Massa alimaliza nafasi ya saba mbele ya dereva wa Lotus Kimi Raikkonen.
Katika majaribio ya kwanza jana Ijumaa Hamilton alimaliza katika nafasi ya kwanza lakini Mercedes wakashindwa kufanya vizuri kwenye majaribio hayo ya pili.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.