Sunday, October 27, 2013

El Shaarawy azigonganisha Chelsea,Arsenal,Spurs....Liverpool yaingilia kati

Mshambuliaji mwenye miaka 20 Stephan El Shaarawy anataka kuondoka AC Milan kwenda kusaka maisha mapya yatakayomfanya kupata nafasi ya kucheza.
 
Maamuzi hayo yanawafanya Chelsea, Tottenham na Arsenal kuingia vitani lakini Liverpool inaelezwa ndio wana nafasi kubwa zaidi ya kuzizidi kete klabu hizo.
 
El Shaarawy alifunga mabao 16 msimu uliopita lakini sasa Mario Balotelli ndio anaonekana kuchukua nafasi zaidi kwenye klabu hiyo huko San Siro.
 
Wamiliki wa Liverpool wanapanga mipango ya kununua wachezaji wadogo na El Shaarawy anaonekana kufit kwenye mipango hiyo.
 
Mshambuliaji huyo anakadiriwa kufikia dau la paundi milioni 25.
 

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.