Tuesday, October 29, 2013

VPL : Mbeya City mwendo mdundo,Yanga yafanya kweli,Simba mmh


Ligi kuu ya soka Tanzania bara imeendelea tena leo kwa michezo mitatu kuchezwa katika viwanja tofauti ambapo katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam, mabingwa watetezi Yanga Africa waliwaalika maafande wa Mgambo kutoka Handeni huko Tanga.

Huko Sokoine mjini Mbeya kulikuwa na mchezo wa mahasimu wa mkoa huo Mbeya City dhidi ya Tanzania Prisons,wakati huko Taboa kwenye uwanja wa Ally Hassan Mwinyi Rhino Rangers wamecheza na JKT Ruvu.

Uwanja wa Taifa Yanga Africa wamefanikiwa kukalia nafasi ya tatu juu ya mahasimu wao Wekundu wa msimbazi Simba kufuatia kupata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Mgambo shooting.

Mabao ya Yanga walitupiwa wavuni na Mbuyu Twite,Hamis Kiiza Diego na Didier kavumbagu.

Ushindi huo umewafanya Yanga kufikisha pointi 22 ambazo ni pointi mbili zaidi ya mahasimu wao Simba wenye pointi 20 ambao jana walikubali kichapo cha mabao 2-1 kutoka wa waoka mikate wa Azam FC.

Mchezo mwingine wa ligi kuu uliounguruma leo ilikuwa huko Mbeya katika uwanja wa kumbu kumbu ya Sokoine mahasimu Mbeya City na Tanzania Prisons walioneshana kazi na matokeo tuliyoyapata kutoka Mbeya timu ya Mbeya City imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 ushindi uonawafanya kuendelea kukimbizana na Azam FC kileleni mwa ligi hiyo wote wakiwa na pointi 23 wakitofautiana mabao ya kufunga na kufungwa.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.