Wednesday, October 9, 2013

Lukaku anataka kumzodoa Mourinho


Mshambuliaji wa Everton Romelu Lukaku amesema anataka kumuonesha kocha wa Chelsea Jose Mourinho kuwa alikosea kumpeleka kwa mkopo kwenye klabu hiyo.

Akionesha kiwango cha juu alipocheza kwa mkopo West Brom msimu uliopita , Lukaku alikuwa na matumaini kuwa angepata nafasi ya kucheza Chelsea msimu huu lakini imekuwa tofauti na akapelekwa kwa mkopo huko Goodison Park.

Lukaku tayari ameshatumbukia wavuni mara nne akiwa na Everton, wakati hakuna mshambuliaji yeyote kati ya waliobakia Stamford Bridge aliyetupia wavuni hata bao moja mpaka sasa.

Anasema ataendelea kuzifumania nyavu zaidi ya Fernando Torres, Samuel Eto'o na Demba Ba.

Anasema anaheshimu maamuzi ya kocha lakini anataka kumuonesha kuwa alikosea kwa kufunga mabao zaidi ya washambuliaji hao waliobaki Chelsea.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.