Tuesday, October 29, 2013
Formula1 : Mercedes yamegeka
Ross Brawn ataacha kuiongoza timu ya Mercedes ya kwenye mashindano ya magari ya langalanga ya Formula One, kufikia mwisho wa msimu huu.
Brawn na timu hiyo ya Mercedes wameshindwa kuafikiana kuhusu wajibu wake katika timu hiyo, kulingana na taarifa za kuaminika kutoka timu hiyo ya mashindano ya magari.
Timu ya Mercedes sasa itaongozwa na wakurugenzi wawili watakaoshirikiana pamoja, Toto Wolff na Paddy Lowe, na vile vile kutoka kwa Niki Lauda, ambaye ni mwenyekiti mkuu asiyekuwa na mamlaka rasmi ya kufanya uamuzi katika kuiendesha timu hiyo.
Mercedes, na hata Brawn, walikataa kuzungumza kuhusu kinachoendelea kati yao.
Hatua ya kuamua kuondoka kwa Brawn inaafikiwa baada ya miezi mingi ya kushauriana na wakuu wa timu ya Mercedes.
Brawn, ndiye aliyechangia umaarufu wa Mjerumani Michael Schumacher kuweza kulinyakua taji la dunia mara saba katika mashindano ya langalanga, wakati alipokuwa mkuu wa timu za Benetton na Ferrari.
Brawn pia alihusika katika ushindi wa Jenson Button, alipoibuka bingwa wa msimu wa mwaka 2009, na alipojisajili kama mtu binafsi asiyekuwa na kampuni, kwa jina Brawn GP , kufuatia timu ya Honda kujiondoa katika mchezo huo. Hatimaye timu ya Mercedes ilimchukua mwaka 2010
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.