Kocha wa Chelsea Jose Mourinho amejipa shavu mwenyewe baada ya mabadiliko aliyoyafanya kuwaingiza Eden Hazard na Willian kumlipa kwa kupata ushindi wa mabao 3-1 kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Norwich City.
Mourinho aliwaingiza Samuel Eto'o, Eden Hazard na Willian na ikamlipa huku akisema unapofanya mabadiliko na mchezo ukabadilika maana yake kocha anastahili sifa zake na kama utafanya mabadiliko na mambo yakawa mabaya maana yake kocha amefanya mabadiliko ya hovyo.
Katika mchezo huo Chelsea walitangulia kutupia wavuni katika dakika ya 5 kupitia kwa Oscar baada ya kazi nzuri ya Demba Ba kabla ya Norwich kusawazisha na baadaye Hazard na Willian wakatupia mabao yaliyowapa ushindi wa kwanza wa ugenini timu hiyo ya Chelsea.
Ushindi huo umewapaisha Chelsea mpaka nafasi ya tatu wakifikisha pointi 14 baada ya mechi saba wakiwa nyuma ya vinara Arsenal wenye pointi 16 sawa na Liverpool wanaokaa nafasi ya pili kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.