Sunday, October 13, 2013

Jembe hili Ozil lingekuwa la Barcelona

MESUT OZILkwasasa ni kipenzi cha mashabiki huko Emirates baada ya kutua akitokea Real Madrid, lakini angeweza kuwa mchezaji wa Barcelona hapo kabla.

Inaelezwa kuwa Barcelona wangeweza kumnasa Ozil kwa paundi milioni 7 tu kutokea Werder Bremen 2010.
Lakini kwa mujibu wa El Mundo Deportivo, Ozil alikutana mpaka na Rais wa klabu hiyo Sandro Rosell ,bodi ya Barcelona ikagawanyika na kuiruhusu Real Madrid kumnasa kwa dau la paundi milioni 13.

Ozil alifanikiwa kuwa mchezaji wa kiwango cha dunia akiwa Madrid na Arsenal wakatumbukia na dau zito la paundi milioni 42 na kumchukua kutoka Real.

Kiungo huyo mwenye miaka 24 tayari ameanza kung'ara akiwa na Arsenal baada ya mechi saba za ligi kuu ya England wakiwa kileleni.
Mapema wiki hii Ozil alimwagia sifa boss wake Arsene Wenger,akisema Mfaransa huyo atamaliza ukame wa mataji msimu huu.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.