Tuesday, October 22, 2013

Evra : Naondoka Man U kwasababu zangu binafsi

PATRICE EVRA ameweka bayana kuwa ataondoka Manchester United mwishoni mwa msimu akisema sababu zake binafsi zinamzuia kusaini mkataba mpya huko Old Trafford.

Evra mwenye miaka 32 ameitumikia klabu hiyo kwa miaka 9 akishinda mataji matano ya ligi kuu na moja la Champions League,lakini sasa yupo tayari kuondoka kwa mashetani hao.

Anasema ameamua kuondoka mwenyewe kwa sababu zake binafsi na hakuna tatizo lolote la kimkataba na Man U kwasababu walitaka amalize maisha yake ya soka kwenye klabu hiyo.

Wakati Evra akishindwa kutoa maelezo zaidi ya jambo hilo,tamko lake linaweza kuwafanya Man U kuzidisha kasi ya kumuwania Leighton Baines wa Everton ambaye walishindwa kumsajili wakati wa usajili uliopita wa majira ya joto.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.