Friday, October 11, 2013

Tevez awachokonoa Man U

Mshambuliaji Carlos Tevez amewachokonoa mashabiki wa Manchester United baada ya kutamka maneno ya kumtaka Nemanja Vidic kuondoka kwenye timu hiyo na kujiunga naye Juventus.

Vidic, ambaye anamaliza mkataba wake na United baada ya kumalizika kwa msimu anawaniwa na klabu hiyo ya Serie A na huenda wakatumbukia katika usajili wa dirisha dogo.

Licha ya kocha David Moyes kusema kuwa atampatia mkataba mpya Vidic lakini Tevez amemwambia beki huyo ajiunge naye huko Turin badala ya kusaini mkataba mpya.

Tevez anasema beki huyo anafaa zaidi katika ligi ya Italia kwakuwa ana nguvu na ni beki mzuri.

United wanataka kumuongeza mkataba wa miaka miwili ikiwa pamoja na kumuongeza mshahara.

Mbali ya Juve pia AC Milan na AS Roma wanatamani kupata huduma ya beki huyo.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.